Elections 2010 Aliyetuhumiwa Kumtukana Kikwete sasa Kugombea jimbo la Musoma Vijijini.......


Big up nakuunga mkono nena kiagata pale tuna tawi na diwani wasaidie maana nami nilisha amua kujitoa mhanga ila sijaombwa pia kuwa mwangalifu mkono alivuruga jimbo lile kwa rushwa anawahonga walevi pombe kiasi kwamba kila tukienda hasa na gari wanadhani u mgombea usijaribu kuwapa pesa za gongo
 

Mkubwa nimekusoma na ninashukuru sana..nivizuri pia ukijitoa mhanga..Unajua kwanini..nampenda sana hayati Dr. Martin King Jr...aliwahisema akiwaambia wamerekani weusi kuwa 'Kama mpaka sasa hakuna mmarekani aliyeona kuwa kuna jambo ambalo yuko tayari kufa kwalo basi hafai kuishi marekani'...Kumbe kujitolea kwako mhanga kunaonyehsa uko Tayari kufa kwa ajili ya Jimbo letu la Musoma Vijijini...Ndo maana nikasema kwa pamoja tunaweza kaka hebu nitextie namba ya simu ya huyo Diwani wetu wa hapo Kiagata....Asante sana kwa kuwa pamoja ndug yangu..
 
kwani hoja yangu imekuwa ngumu sana kujibika??, or u need more time?
 

Kaka nashukuru na ninakuahidi kuwa nitakuwa mwaminifu na nitasimimamia maneno yangu ondoa shaka...Ukweli sina maana ya kuwa nimekubalika kupita watu wengine mpaka kufikia kuombwa kugongea...Hii inatokana na watu walioona courage yangu kule Temeke na kwamba wanahitaji mbunge wa aina hiyo...sasa yawezekana kabisa CDM isiniteuwe na ikateuwa mtu mwingie kwan wako wengi wenye sifa na uwezo mkubwa wa uongozi hivyo kama sio mimi basi nitamsaidia atakayeteuliwa na CDM.
 
kwani hoja yangu imekuwa ngumu sana kujibika??, or u need more time?

Kaka siko katika kupimwa kuwa nafaa au sifai..nilichofanya nikuujulisha UMMA kuwa nimekubali kwa hao wachache niliozungumza nao na kusoma text zao kuwa nimekubali kugombea kama Mwenyezi Mungu atatupa uzima,hata hivyo nikasema nitaendelea kupambana nikishirikiana na wapenda maendeleo wote ili kuhakikisha tunaleta (WOTE) maendeleo endelevu..Sasa naomba niijibu hoja yako wakati huo ukifika ambapo kwanza wanaCDM watakuwa wanateua wagombea....
 

Nimependa sana majibu yako mkuu-yametulia. Tuko pamoja, na daima kwa pamoja, tutafika.
 
CCM-CCK-CDM-CCM-CDM-?

sorry, naomba kuuliza,

unataka utuambia kuwa sasa utakuwa na msimamo, au msimamo wako ni popote upepo unapoelekea?

Dadangu Judith,

Inawezekana ukawa umenichanganya...sijawahi kuwa CCM-CCK-CDM-CCM-CDM...Ila ni ukweli usiopingika kuwa nilikuwa CCM na nikatoka nikawa CCJ ambayo nilikuwa mmoja wa viongozi wake wajuu kitaifa. Hata hivyo CCJ ilifanyiwa mizengwe na hivyo kutokuqualify kupata usajili..Baada ya hapo, tulitoa tamko la kuunganisha nguvu na CDM na hivyo ndivyo ilivyo so sijawahi kutoka tena CDM tangia hapo....Nimekuwa na msimamo huo na sitarajii wala sitegemei kuubadili. Sasa CCK ni baadhi ya wale ambao hawakwenda CDM, nasikia kwa ushauri wa mzee Tendwa wakaamua kuanzisha Chama kingine kinachoitwa CCK....Sasa sijui kama nimekujibu ipasavyo dadangu...
 
Una dalili za kuwa mbunge, tusubiri ridhaa ya wananchi maana CDM ni chama cha watu cyo chama cha chama, Hope u got me
 
Nakutakia kila la kheri. Lakini naomba pia ufahamu nguvu ya fedha ya Mheshimiwa Mkono. Tatizo watu wengi wamezoea 'lamba lamba' hasa wakazi wa vijijini.

Mpaka nakubaliana na ushawishi wa kugomea ujue nimefanya utafiti wa kina na nina hakika kwamba, kama Mwenyezi Mungu atanijalia uzima na afya njema na kama CDM kitaniteua niwe mgombea na mwisho tume ikaniteuwa..ninahakika ya ushindi coz udhaifu wa mkono ninaufahamu licha ya kuwa anapesa za kufa mtu...Usihofu ndugu yangu tuko pamoja..
 
Mkuu,..
heshima kwako!

nina maswali mawili na maoni/doughts pia
maswali:
1.Kwanini hauta gombea temeke tena au umeona uwezekano wa kushindo ndo basi tena?
2.mara ya mwisho ulikua musoma vijijini lini?
3.kesi yako imeishia wapi?

doughts...
1.sidhani kama wananchi wa musoma vijijini wame mchoka mkono kiasi hicho,
ana daiwa kuwa fisadi,lakini ni fisadi anae leta maendeleo sana katika jimbo lake.
kila mwana msm vijijini na hata mjini analijua hilo,...labda kama atakua hayupo au hatagombea ndo utashinda!

2.Nime zaliwa mwanza,ila std1-7 nimesomea musoma vijijini,tarafa ya kiagata,kata ya bwiregi na kijiji cha masurura,...
na shule ya msingi masurura!
katika mda nilio soma huko,toka mkono alipo kuwa mbunge ame badilisha mambo mengi sana hadi kujiwekea uhakika wa
kushinda kwa kishindo hata asipo piga kampeni!
Kwanini unadhani utashinda au kwa sababu ndugu zako wame kuita huko?

3.kuna mgombea alokua huko alijitoa,na ina daiwa ni kwa sababu mkono alimpa chapaa kibao na ukawa mtaji wake,
hii ni kwasababu mkono hakutaka shida ya kuzunguka na kampeni ingawa alikua na uhakika wa kushinda,...
je,na wewe umependa dau la mkono hadi ujitokeze kwenda kugombea huko?

All the best mkuu,...
 
Mimi naunga mkono miguu na mikono; maana tusibaki kuongelea pembeni mikia chini ya kitovu na mara mtu mwingine anapodiriki kujitokeza hadharani tunaanza kumvunja moyo ili naye afyate mkia kama mbwa koko!

Nilishawahi kusema huko nyuma ili cdm ifike huko vijini kwa urahisi ni lazima tupate watu wenye nia ya kugombea maeneo yale ili waanze kazi ya kukijenga chama na kuweka mahusiano mazuri na watu wale.
Mabo ya kupeleka sura zetu 2014 eti tunataka kura haitaKuwa. Mtu anayetaka kugombea ni lazima awekeze siyo chini ya miaka mitatu akifanya kazi ya kukijenga chama kwa kuwa na watu wenye ushawishi kila kona ya jimbo na wanachama waaminifu watakao kitanganza chama

Mimi nashauri chadema iwaruhusu watu ambao wana nia ya kugombea waanzenze leo kazi hiyo na sikusubiri utaratibu wa chama kama wanamagamba. Lazima cdm ilichukulia swala la kugombea ni haki ya msingi na kila mtu anaruhusiwa ni kazi yake kwenda kujiuza na kukubalika kwa wananch hiyo siyo kazi ya uongozi wa cdm.

Kama kuna watu zaidi ya mmoja wanataka kugombea jimbo moja iwe ni kazi yao kujiuza kwa wananchi mpaka wakati wauteuzi utakapo fika.
Mimi naamini mtu atakeye fanikiwa kukijenga chama pia atakuwa amekubalika na hakutakuwa na sababu ya kutompitisha kugombea ili hali amekiletea faida pia chama.
Pia itakuwa rahisi kwa watu kuwachuja hawa wagombea maana watakuwa wakishirikiana nao kwa muda mrefu zaidi kuliko ilivyo sasa mtu anaweza kutumia lambalamba kwa muda mfupi akwateka watu. Lakini hawezi kutoa lambalamba kwa muda wa miaka minne mfululizo hata kama yeye ni tajiri atachoka tu.

Tukumbuke mtu mwenye nia yakuwaletea watu mabadiliko ya kweli na sikupata jimbo, hachoki hata akishindwa bado ataendelea kushirikiana na hawa watu mpaka watakubaliana naye maana ataendelea kutimiza ahadi zake hatakama ameshindwa.

Once again mimi na unga mkono na kama kuna mtu mwingine anataka pia kupambana na huyu brother ni ruksa ajitokeze pia wakati huu maana mwisho wa siku ni wananchi ndo wanaamua ni yupi anawafaa na siyo uongozi wa cdm.

Haya ni mshambulizi mazuri kwa wana magamba kabla hawajaanza kuchakachua ni lazima wajue kabisa 2015 cdm siyo tena mambo ya kuzima moto kama vyama vya akina DOVUTWA.
 

Naona unajisifia kuwa ulimtukana kikwete, huji hiyo ilipunguza kura zako Temeke? Pia hujazungumzia kuwa uligombea ubunge Temeke, huoni hiyo itachanganya watu wadhani ni yule aliyehongwa akampitisha mkono bila kupingwa?
Pia hujasema kura ulizopta Temeke ili tujue nguvu yako kisiasa katika jimbo ambalo hukujiandaa?
 
wewe ulitegemea uje hapa halafu tukuchekeee tu kwa sababu unagombea ubunge kwa kupitia chadema? kwanza mpaka hapa wewe jamaa ushaukosa ubunge, hujaja na strategic gani ambazo utazitumia ili kuwakomboa wananchi wa kigoma . so we can say kuwa wewe ni useless kwanza kitendo cha kumtukana rais wewe unachukulia kama ni sifa? hufai kabisa kuwa chadem kwenye chama makini .njoo kivingine ila sio kujisifia eti kwa kuwa unatuhumiwa kumtukana rais. we dont know you.
 

Mheshimiwa Speaker, nashukuru kwa maswali yako ila sidhani kama ni busara kuyajibu sasa...hebu ngoja nikijenge CHAMA kwanza kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wana CDM. Na pia nashukuru kwa daut zako coz kama mwanadamu una haki ya ku-dought na nimezipenda sana na wakati ukifika,WanaCDM wakanipa ridhaa na Tume ikaniteua nitakuprov wrong na hata kama sikuteuliwa mimi,akateuliwa mwanaCDM mwingine,nitafanya naye kazi bega kwa bega ili kukuprov wrong juu ya imani yako kwa Mkono...Naomba kuwasilisha mkuu..
 

Mh. Ivuga, nashukuru sana kwa mchango wako coz uko na uhuru wa kusema chochote unachoweza bila kuvunja shria za nchi...Na hapa kusema ukweli haujavunja shria yeyote...Labda nikusahihishe kuwa sio Kigoma ila ni Musoma Vijijini...Ubarikiwe sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…