JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Tazarn Alfan Mwambengo (27), mkazi wa Ukonga, ambae anatuhumiwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu kifo cha Dkt. Harrison Mwakyembe kupitia chaneli ya televisheni ya mtandaoni jambo ambalo si la kweli.
Katika chaneli hiyo ya mtandao mtuhumiwa huyo aliandika, “BREAKING NEWS HUZUNI YATANDA MAZISHI YA MWAKYEMBE” taarifa ambazo ziliibua taharuki kubwa kwa wananchi hasa kwa Dkt. Mwakyembe mwenyewe na familia yake.