Misingi ya ndoa imeharibika. Wewe waweza ingia kwenye mahusiano sababu ya upendo na uhitaji wa kupata msaidizi, lakini yeye akawa ameingia kwenye mahusiano na pesa zako au mwili wako.
Baada ya muda mambo yakibadilika anakinai mwili wako, anapata pesa zingine sasa zile zako hazionekani tena inaingia chuki ndani ya moyo na mambo yanakua si mambo
Mungu atusaidie turudi kwenye mpango wake ili
Kila Mume Na AMPENDE mke wake
Kila mke na AMTII mume wake
WAEFESO 5: 22-30
Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.
Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa. Kwa kuwa u viungo vya mwili wake.
1WAKORIONTO 7: 1-5
"Na sasa kuhusu mambo mliyoniandikia. Ni vizuri mtu asioe. Lakini kwa kuwa dhambi ya zinaa imeenea, kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.
Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe; na hali kadhalika mke kwa mumewe. Kwa maana mke hatawali mwili wake mwenyewe, bali mume wake ndiye autawalaye. Vivyo hivyo, mume hatawali mwili wake mwenyewe, bali mkewe ndiye anayeutawala."
MUNGU ATUSAIDIE