Aliyeua wenzake akiwa amepandisha mapepo, anakosa kisheria?

Medical examination on mental health

Sent from my HUAWEI G730-U10 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, kisheria mtu huyu anakuwa kwenye insanity interval -epileptic fits. Huyu hata akitenda kosa kuna defence yake, kwa vile anahesabika hakutenda kwa kukunuia (hakuwa na mens rea). Lakini defence hii itahitaji kudhibitishwa, kwanza na mkosaji mwenyewe na vilevile wataalam wa afya ya akili, kwamba wakati kitendo kinafanyika mkosaji alikuwa hatambui anachokifanya, na anayo maradhi hayo.
 
so ameua bila kukusudia au..
 
Ah! Kumbe na hawa wanapandisha nilifikiria wale tu wanoambiwa dini majini
 
Tumesafiri watu watano baharini. Chombo chetu kikapigwa dhoruba.
Tumekaa chomboni kwa siku sita bila msaada
Tukakubaliana tujile nyama.
Tukapeana namba (1-5). Mwenye namba 1 akaanza kuliwa.
Zoezi likaendelea hadi namba 4. Nikamla. Nikabakiza nyama. Nikaishi kwa siku Tatu nikaokolewa.
Baada ya siku kadhaa ndugu wa marehemu wakanifungulia charge ya kuua.
Nikaweka advocate .Mahakama ikaniona Nina hatia yakuua bila kukusudia kwani nilikuwa naokoa maisha.
Wafiwa waka appeal kuwa kwa nini sikufa mie?
Kesi IPO Mahakama ya rufaa inaendelea.
 
Sasa shida hayo sio maradhi ni mapepo, inamaan hata mtaalam wa afya hawez ku examine maan hana tatizo kisayansi lkn ki roho....na hamna defence ya mtu spiritual wise, insane will only stand when proved by medical tests, huyo sijui io defence wana iprove vipi

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Hajaua bila kukusudia. Kuua bila kukusudia ni jinai inayojitegemea. Hapa atadhibitika kuua, lakini mahakama haitamtia hatiani sababu alifanya kosa akiwa insane
Insane ni lazima iwe examined by medical tests ili ukatolewe ushahidi kuwa mtu ni insane.....sasa kmbuka mapepo ni ugonjwa hauwez onwa kwa vipimo vya kisayansi sasa hiyo defense haitoweza kuwa proved kimahakam maan hawaamini spiritual wise

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Na ndio maana itabidi wataalamu wa afya ya akili wathibitishe kuwa wakati tendo linafanyika mtuhumiwa hakuwa katika akili yake. Kinachoangaliwa hapa sio hayo mapepo, kinachoangaliwa ni state of mind.
Tatizo lolote linapomkumba mtu likaharibu uwezo wa akili yake kutambua 'nature of the act' basi hilo huchukuliwa kama ni chanzo tu kisababishi cha action aliyofanya mtu, lakini sheria inazingatia zaidi state of mind wakati wa tendo jenyewe. Kisheria, hata kichaa au mwenye mtindio wa ubongo anaweza kushtakiwa na kuhukumiwa kwa jinai ikiwa itathibitika kafanya kosa akiwa anafahamu nature ya kosa jenyewe, hii inatokea palek mgonjwa wa akili au kichaa anakuwa kwenye kitu inaitwa 'lucid interval'.
 
cheki post juu hapo
 
Huwezi Kuwa Exempted Absolutely From Criminal Liability Unless Uwe Hujaua Kabisa. So As Long As Umeua Utetezi Wowote Utakaoutoa Kama Ukikubaliwa Utashusha Kesi Toka Kuua Kwa Kukusudia (Murder) Kiwa Kuua Kwa Kutokukusudia (Manslaughter). Hapo Anatakiwa Athibitishe Kuwa Alikua Insane (Defense Of Insanity) Wakati Anaua.La Sivyo NGOMA NAGWA!

Sent from my HUAWEI Y530-U00 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…