Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,606
- 6,672
Askofu Joseph R. Mlola, ALCP/OSS, wa Jimbo Katoliki Kigoma anasikitika kuwajulisha kuwa ndugu yetu Padre Raymond Saba, ameitika sauti ya Mungu kutoka dunia hii leo kama saa mbili kasoro dakika ishirini hivi usiku.
Kama tulivyowajulisha, alikuwa akipatiwa Matibabu katika hospitali ya Rabininsia.
Tuzidi kuiombea roho yake pumziko la milele kwa Mungu.
Tuwaombee wazazi na jamaa zake wote. Tushikane mkono katika kipindi hiki kigumu kwa kuombeana.
Taarifa nyingine tutajulishwa baadaye.
Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie. Apumzike kwa amani. Amina.
Fr Evarist Guzuye Chancellor
Kigoma, 3 Agosti 2021
NOTE: Huyu ndiye alikuwa Katibu Mkuu wa TEC aliyenyang'anywa pasipoti baada ya kupata msukosuko kufuatia waraka wa Kwaresima mwaka 2018.