Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Vijana NCCR Mageuzi aliyeripotiwa kupotea aokotwa Porini akiwa Mahututi

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Vijana NCCR Mageuzi aliyeripotiwa kupotea aokotwa Porini akiwa Mahututi

Enzi za Jiwe watekaji walikuwa wakipongezana bar jioni.
Sasa hivi Samia alishaukataa huo uharamia. Walio chini yake kwakuwa ni machawa lazima waucheze mchezo wake
Vipi wale vijana waliopotea pale Kariakoo Samia vipi hahusiki hapo? N vipi yule askofu mstaafu wa Angalikani Mwanza alipatikana amefariki na mwili wake kutubwa ziwani Samia hahusiki? Nyinyi ni kikundi cha wapuuzi tu matukio yako miaka yote!
 
Mambo ya kutekana hayajaanza leo wala jana
Haya mambo yatakuwepo na kuendelea kuwepo

Ova
Na huo ndo ukweli sema watu siku hizi wanapenda kujifanyisha kusahau kana kwamba matukio hayakuwepo kabisa yalianza awamu ya tano na sita! Kikwete mwenyewe Dr Ulimboka alitekwa!
 
Huyu kijana anaitwa Clinton, na kulikuwa na taarifa humu siku chache zilizopita kwamba amepotea na hajulikani alipo.

Taarifa za sasa zinaonyesha kwamba amepatikana akiwa hoi bin Taaban huko porini alikotupwa .

Taarifa zaidi zinakuja
Vijana siku hizi wanatembea na wake za watu, labda kafumaniwa
 
Umemkumbuka jinsi enzi zake walivyotekwa kina Mo, Roma nk
-%20KumbukiziMTAFUTANO.jpg
 
Vipi Dr Ulimboka alipo okotwa Magwepande alikuwa yule jamaa pia anahusika? 😀 😀
Yule jamaa ana damu ya kunguni, hata uuzwaji wa zile nyumba lawama zote alibebeshwa yeye wakati alikuwa na wakubwa zake. Yule jamaa ni kamaa.............kwa jins alivyobebeshwa dhambi za watu.
 
Acheni kuhamisha magoli. Kule NCCR kuna genge linamtoa Mbatia kwenye Uongozi kwa figisu na kuna moto unawaka chamani. Huyu mtu amepotea tangu alipoenda Kisutu kwenye kesi ya kumng'oa Mbatia madarakani. Hebu unganishen dots.
Halafu hivi vyama vyetu vinaua makada wake vinasingizia wasiojulikana.
CHACHA WANGWE alitaka kumtoa MBOWE uenyekiti yuko wapi? Na yule kijana wa Kichagga MALYA aliyetekeleza mauaji mkampa Cheo.
Je, Mlinzi wa Mbowe aliyenyongwa gest pale Temeke?
Tuache porojo kuna facts zikiwekwa hapa hata hao kina JPM mnaowasikizia mtawaona malaika.
RIP Mhe.Mtikila
Huna lolote na hujui lolote
 
Wewe hujui kitu! Wakati Dr Ulimboka anatekwa ulikuwa utawala gani vile? Kwa hiyo kila ubaya mnajificha kwenye kivuli cha JPM! Mkosoeni Samia!
Ilikuwa utawala wa mtu mwema asiyekufa.
 
Huyu kijana anaitwa Clinton, na kulikuwa na taarifa humu siku chache zilizopita kwamba amepotea na hajulikani alipo.

Taarifa za sasa zinaonyesha kwamba amepatikana akiwa hoi bin Taaban huko porini alikotupwa .

Taarifa zaidi zinakuja
Lete khabari kamili yupo hospital gani tukampe pole!
 
Huna lolote na hujui lolote
Nimekwambia anza kutumia dozi ya akili unarukaruka tu utadhan maharage yako jikoni. Siku ukiminywa na hao unajifanya chawa wao ndio utaelewa na muda utakua ushapita.
 
Back
Top Bottom