Aliyewashonea nguo taifa stars mungu anawaona

Aliyewashonea nguo taifa stars mungu anawaona

Daa..ndio fashion mzee wangu,

Kama nyie mlivokua mnavaa siluali zenu kaa za amita bachan
 
Kwanza kwenda na masuti kwa watu ambao hawajozoea kuvaa suti ni ushamba. Hili ni kombe la Afrika ambayo kila nchi ingebidi iingie na mavazi ya kitamaduni. Kuna mavazi ya kigogo, kisukuma ama kimasai wagewatafuta wangeitangaza vyema nchi sasa haya masuti oversize na viau kachumbari?
Umeandika ukweli mkuu. Suti ni ushamba bora wangeshona mashati ya vitenge. Suti zinafahamika sana duniani na huvaliwa kwenye shughuli nyingi kama ofisini, harusi na mikutano ya viongozi wa mataifa ya dunia japo wengine huvalia kidamaduni. Kama si mvaaji wa suti mara kwa mara unaweza kuonekana mshamba kwani suti inaweza isikupendeze na kutulia mwilini. Suti ina tabia ya kumpendezesha mtu au kumchukiza kutokana na umbile la mtu na mashono ya mtu
 
Kuna Suti za kizee na suti za vijana.Suti za vijana zinaenda na mitindo mipya ya suruali za vitambaa. Kuna Suruali za kubana nyembamba vijana wanaziita modo ndizo vijana wa kisasa huzipenda. Vijana Wanachuo wale wa maofisini wanavaa sana. Ila Mzee ukivaa suti ya modo watakushangaa. Modo ndiyo mtindo wa vijana wa kisasa. Uzuri Wa Suti Uivae Siyo Ikuvae
 
Kawaida ya wachezaji Wa mpira Wa miguu huwa hawapendezwi na nguo za kawaida
 
Walitaka wavae kama ile ya kiongozi wa mjengoni pale dodoma.
 
Kwanza kwenda na masuti kwa watu ambao hawajozoea kuvaa suti ni ushamba. Hili ni kombe la Afrika ambayo kila nchi ingebidi iingie na mavazi ya kitamaduni. Kuna mavazi ya kigogo, kisukuma ama kimasai wagewatafuta wangeitangaza vyema nchi sasa haya masuti oversize na viau kachumbari?
Hivi ule mpango wa vazi la taifa uliishia wapi au wadau walishapiga hela wakatulia ?
 
Back
Top Bottom