Tatizo letu kubwa ni ushabiki wa kisiasa kiasi hata tunashindwa kutumia logic.
Aliyeiua CUF ni maalim Seif kutokana na ubishi, ujuaji na ujeuri aliokuwa nao. Niwakumbushe kidogo.
Baada ya kuhitilafiana kwake na Mwenyekiti wake Profesa Lipumba, Mwenyekiti huyo aliandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.. Maalim Seif kama mtendaji wa chama alipaswa kuwasilisha barua hiyo kwenye kamati kuu ya chama ili iridhie hilo.
Hili hakulifanya kutokana dharau aliyokuwa nayo kwa kujiona kuwa yeye ndiye CUF. Baada ya mambo kuyumba baadhi ya wanachama walimuomba professa arudi naye akakubali. Kwa vile chama hakiku-respond kule kujiuzulu kwake, yeye aliandika barua ya kurejea na hapo maalim baada ya kutumia busara akatumia jeuri na mwisho wa siku mambo yakaharibika kabisa. Hapa wa kumlaumu ni CCM? au upuuzi wa uongozi wa CUF uliojaa dharau na kiburi???