Aliyoyafanya Sadio Mané katika kijiji chake

Aliyoyafanya Sadio Mané katika kijiji chake

Tanzania tuna Bilionea anaitwa Diamond platinum, vitu pekee anachojivunia kijamii ni kubadilisha wanawake, kufanya tafrija za ufuska na kubadilisha magari.

Kuna kitu kikubwa mnoo cha kujifunza kutoka kwa Sadio Mane, Samwel Eto, Nwanko Kanu.
Binadamu hawawezi kufanana, mwache afanye anachotaka..pesa ni zake
 
Wengine wanajenga nyumba za ibada. Inashangaza sana lakini ndiyo ukweli huo
 
▶ Amejenga shule yenye thamani ya €270,000.
▶ Amejenga hospitali yenye thamani ya €530,000.
▶ Hupatia kila familia €70 kila mwezi.
▶ Hutoa nguo bure kwa watoto.
▶ Upatikanaji wa mtandao wa 4G kutokana na ushirikiano wake na Orange.
▶ Kituo cha mafuta kupitia Oryx Senegal hivi karibuni.

View attachment 2263824
Sasa huyu ndio tajiri mwenye hekima. Sio unakaa unajaz magari ya kifahalinambayo hayana impact yoyyote ukiondoa kujilisha upepo tuu
 
Tanzania tuna Bilionea anaitwa Diamond platinum, vitu pekee anachojivunia kijamii ni kubadilisha wanawake, kufanya tafrija za ufuska na kubadilisha magari.

Kuna kitu kikubwa mnoo cha kujifunza kutoka kwa Sadio Mane, Samwel Eto, Nwanko Kanu.

Mkuu Domo sio Bilionea, ni msaka tonge tu kama wengine, usibabaike na nguvu nyingi anazotumia ili tumuone yeye Bilionea, Yale ni matatizo ya akili yanamtesa.
 
ni mambo ya kawaida sana hayo kulingana na uwezo alionao. Yawezekana yote ameyafanikisha kwa hela alioingiza ndani ya mwezi mmoja tu.
 
Halafu jamaa anatumia simu ya kitochi a.k.a kiswaswadu
 
Siyo kupendana shida ni kwamba mtu wa Afrika Magharibi akitajwa kua ni tajiri anakua ni tajiri kweli wakati hapa bongo mtu anakua tajiri akiwa na nyumba na IST
Kama mondi vitu vingi ni udalali wa kutumia jina lake tu sio vyake
 
Kwa hiyo unachagua vile -ve tu ndio unaandika?

Huoni msikiti aliojenga Kigoma, Kulipia kodi watu 500, kuwekea vijana wa bodaboda takribani 1000 full tank kila mmoja, kuajiri vijana wenzake, kufunguza watu kipindi cha ramadhani, kuwapa vijana mitaji n.k

Ulichochagua wewe kuona ni -ve tu, swala la kubadilisha wanawake hakuna Mwanaume awaye yeyote asiyebadilisha wanawake, ni vile tu sisi wengine hatuonwi kwa kuwa sio mastar, huku Uyole Mbeya viwembe tupo wa kutosha tu.

Msipangie watu matumizi ya pesa zao, walitafutia juani waacheni watumie vile wanapenda, ukipata wewe pesa nenda kafanye kama Sadio Mane.

Kuhusu tafrija za ufuska nadhani bado hujaona, nenda Tabata ukaone orgy zinapigwa live ndo utajua Diamond cha mtoto tu.
Ule msikiti wa ujiji hakujenga yeye, alienda kufanya finishing tuu
 
Mbona Samata kajenga msikiti Kigambo huku baba yake anaishi uchochoroni Mbagala.
 
Huyu angekuwa bongo wange mwambia ana show off,wabongo tunanongwa husipotoa utaambiwa mchoyo au masharti ya mganga wake.
 
[emoji666] Amejenga shule yenye thamani ya €270,000.
[emoji666] Amejenga hospitali yenye thamani ya €530,000.
[emoji666] Hupatia kila familia €70 kila mwezi.
[emoji666] Hutoa nguo bure kwa watoto.
[emoji666] Upatikanaji wa mtandao wa 4G kutokana na ushirikiano wake na Orange.
[emoji666] Kituo cha mafuta kupitia Oryx Senegal hivi karibuni.

View attachment 2263824
Hakika amefanya makubwa
 
Back
Top Bottom