MIMI BABA YENU
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 305
- 728
Katika miaka hii mitano ya Serikali ya Awamu ya Tano kazi kubwa imefanyika. Sisi kama Serikali tumetimiza wajibu wetu, tunaiona nchi yetu inaendelea kupata maendeleo kwa kasi
Serikali hii imehamasisha sana watu kulipa kodi na sio kulipa kodi tu bali waione thamani ya kodi wanazolipa, tulipoingia madarakani tulikuta makusanyo ya kodi kwa wastani yakiwa TZS Bil. 850 lakini sasa tunakusanya TZS Tril 1.5.
Ugonjwa wa Corona umekuja wakati ambao tuna mambo mengi tumeyapanga kama nchi, kuna hatua nyingi za kujikinga tulizichukua. Kwa upande wetu zipo athari za kiuchumi ila sio kubwa sana.
Uchumi wetu haujawahi kushuka kwa miaka 10 iliyopita, ni malengo yetu kwa kipindi cha kati na muda mrefu kwamba uchumi ukue kwa zaidi ya 6%, kama tukiendelea na ukuaji huu, kwa takwimu za Benki ya Dunia huenda mwakani tukaanza kuingia kwenye uchumi wa kati.
Huwezi kupata maendeleo ya watu bila kuwekeza kwenye vitu, Awamu ya Tano tumewekeza sana kwenye vitu tukiamini vitachagiza maendeleo ya watu kwa kuwapatia utaalamu, Ajira kipato n.k
Kila sekta ambayo Serikali imewekeza inachangia katika kuleta mageuzi kwa wananchi wa kawaida, miradi yote mikubwa ya Serikali imeajiri watu. Kwa takwimu zilizothibitishwa sekta ya viwanda pekee imeajiri watu zaidi ya 200,000.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli anasisitiza dhana ya mabadiliko ya kifikra, uchumi jumuishi utafikiwa sio tu kwa Serikali kuendelea kuwekeza katika miradi mbalimbali bali ni kwa Watanzania kuelewa na kutekeleza dhana ya kufanya kazi kwa bidii.
Mradi wa bomba la mafuta haujafa, ni wazo ambalo viongozi wetu wamelipigania hivyo ni lazima litekelezeke, kwa Tanzania hatua nyingi tumeshamaliza kwenye mwezi Julai, 2020 Tenda zitaanza kutangazwa.
Tunawashukuru mashabiki wa michezo kwa kuzingatia kanuni na miongozo iliyowekwa wakati wa michezo kipindi hiki cha mapambano dhidi ya Corona.