Uchaguzi 2020 Ally Bananga atia nia ubunge Arusha mjini - CHADEMA

Uchaguzi 2020 Ally Bananga atia nia ubunge Arusha mjini - CHADEMA

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

2452348_IMG-20200710-WA0023.jpg

Mwanasiasa maarufu nchini na aliyekuwa diwani wa Sombetini jijini Arusha kupitia CHADEMA Ally Bananga a.k.a Binamu Bananga ametia nia ya kugombea ubunge Arusha mjini kupitia CHADEMA.

Kwa wanaofahamu siasa za Arusha wanajua hili ni jaribu kubwa sana kwa CHADEMA kuonesha ukomavu bila kuivunja rasmi ngome yao kuu ya upinzani jijini Arusha na kufanya CCM ishinde kirahisi kuliko uchaguzi wowote uliowahi kufanyika Arusha.

Inawezekana kuna kundi kubwa la madiwani/wanachama wanaotaka kufanya kazi na mtu mwingine na wamemtuma Bananga kutuma ujumbe wao. Sasa unahitajika ukomavu mkubwa kuvuka hili bila kupasua chama.

Binafsi naona Ally Bananga ni mwanasiasa mkomavu anayeweza kushirikiana na wananchi, wanachama, madiwani na serikali kuletea maendeleo wananchi tofauti na Lema ambaye harakati zake zinafaa kutafutiwa kazi zingine za chama na nafikiri kuwa kiongozi wa kanda inatosha.

Kila lakheri Ally Bananga, operations zako kama diwani na kiungo muhimu wa CHADEMA na wananchi hapo Arusha unastahili kumpokea kijiti Mh. Lema maana unajua shida za wana Arusha kiuhalisia zaidi.
 
Mbowe kazi anayo,atakuwa tayari kumpiga chini Lema ?????Lema aliyepokonya laptop ya kina MM,hadi nasi tukausoma waraka.
Huu ni mtihani ndugu yangu. Usisahau katibu mkuu ni Mnyika na si mtu wa sarakasi otherwise itakuwa ni kuziba pancha jimboni na makao makuu [emoji41]
 
Hongera kwa muhusika, baraka za Jah ziwe juu yake.
 
Ni ile tu wanasiasa ni wabinafsi mno, Lema angeweza kujijengea heshima kubwa kabla hata ya vikao kuamua, angemuunga mkono Bananga naamini agekuwa kiongozi wa kanda mzuri sana. Kwanza ameshaongoza miaka 10, hiyo ni heshima kwake tena kubwa, pili ni Kiongozi wa Kanda kwa sasa. Hivi kwanini atake na ubunge pia wakati MTU mwenye sifa kama Ally Bananga yupo? Anyway mie so mkazi wa Arusha, ila busara za viongozi zitumike
 
Back
Top Bottom