Ally Bananga: Mdude Nyagali anatakiwa kupumzika kwanza, kumpatia kipaza sauti mapema sioni tukimpenda na kumsaidia

Ally Bananga: Mdude Nyagali anatakiwa kupumzika kwanza, kumpatia kipaza sauti mapema sioni tukimpenda na kumsaidia

Yupo mwingine anaitwa tito magoti,, huyo alikua akijifanya kutetea haki za binadamu na NGO,fulani hivi,,nae ameanza kutoa vitisho vya kisiasa,,yaani keshakuwa mwanasiasa na anatoa kauli za kushuritisha mamlaka,,"namuangalia tu...huwezi kuwa msaliti,halafu......"
Mbonà unakuwa juha, Hawa wanatetea demokrasia, kosa liko wapi?
 
Ukiwa ni mtendaji mkuu wa chama taifa,mipango yote hupata baraka kupitia ofisi yako.

BAVICHA waliandaa "KATIBA DAY"ni jambo jema sana kitaifa kupitia BAVICHA.
Kitendo cha MDUDE kupewa nafasi nakuongea upumbavu nje ya mada haikubaliki.

Nakuomba kaa na vijana wako uwaelimishe mipaka ya uwasilishaji.
 
Kwa hiyo unafikir wew hutokufa! Mjifunze kuelewa kwamba watu wana character tofauti. Mdude ndo alivyo! Jitahidi kumtafsiri kwa kutumia hulka yake, na siyo kwa kutumia utashi wako. Yeye ndo yuko hivo, hayo uliyoshauri anaweza kuyapata akiendelea na harakati zake.
 
..hicho anachopendekeza ali bananga labda kinawezekana ktk awamu hii ya rais samia suluhu.

..wakati wa rais magufuli walikuwepo wakina joseph selasini, james mbatia, prof.lipumba,...ambao walikuwa na mtizamo kama wa ali bananga lakini bado hila na ukatili wa ccm dhidi yao zilikuwa palepale.
Waliusoma upepo mapema! Sometimes shari zinaepukika ukitumia akili na hekima kidogo tu
 
Amevurugwa anaongea utumbo mtupu.
 
Ni kweli maneno ya Mdude hayapendezi. Lakini mnapata wapi moral authority ya kumnyooshea vidole wakati maneno mabaya kuliko haya yalitamkwa dhidi ya viongozi wa upinzani hadharani na mlikaa kimya? Watu wametukanwa bungeni, watu wametishiwa maisha yao n.k. lakini mlikaa kimya ama mlishangilia. Mdude amewekwa ndani kwa tuhuma zisizo na mashiko lakini hamkusema kitu. Waliokuwa wakipiga kelele kumtetea ni wale mliowakejeli kwa kuwaita wanaharakati. Ni wangapi kati yenu, pamoja na huyo mheshimiwa wa Arusha, mliwahi kwenda kumtembelea yeye na wenzake gerezani na kujitokeza Mahakamani zinaposikilizwa kesi zao? Na mnajua kuna wangapi bado wako ndani wakingojea hatma zao?

Katika demokrasi kamili uhuru wa kumkosoa kiongozi wako hata kwa lugha ambayo hataipenda ni sacrosant. Kipimo cha demokrasia ni hatua gani zinazochuliwa dhidi ya watu kama Mdude na sio wangapi wanaimba mapambio kuwapongeza viongozi. Kiongozi ukisikiliza vilio vya watu kama Mdude utafaudika sana kuliko kuwasikiliza wale ambao kila kukicha ni kukupamba.

Amandla...
 
Yaani mtu aliyefanya atoke ndiye amfanyie kauli za dharau hivi?

Unajua serikali inaweza kukata rufani na kesi ikapitiwa upya kwa maelekezo?

Mtu akishauriwa muwe mnaacha kumvimbisha kichwa wakati nyie ni waoga kama tumbili
Bananga anataka kusema Mdude alikuwa mgonjwa wa akili kabla hajapelekwa jela? au amekuwa mgonjwa wa akili baada ya kutoka jela?

Mdude jana hakumtukana Rais, ni kauli aliyoitoa ndio imeonekana kuwashangaza/shtua wengi, japo nina hakika wengi wenu mkiambiwa muoneshe tusi kwenye ile kauli hamtaweza, mnatumia hisia zaidi kuhukumu.

Mmekuwa mkifikiria hili jambo kwa upande mmoja tu, kwanini hamfikirii na mateso aliyopitia Mdude akiwa gerezani muda wote huo kwa makosa ya kubambikiwa?

Nae ni binadamu, ana hisia, muacheni atoe frustrations zake, badala ya kusema akajifungie ndani huku sheria za nchi zikiendelea kuvunjwa, na mvunjaji ndio mnamlinda kama malaika, mnamvimbisha kichwa azidi kujisahau aendelee kufanya apendavyo.

Ikulu ni ofisi ya umma, na yeyote anaekaa pale ana jukumu la kuwatumikia wananchi bila kujali itikadi zao, usawa na haki viwepo kwa wote, akijisahau kwa hilo ni lazima akumbushwe, mahaba yenu kwa "mama" yatazidi kumuharibu, amkeni.
 
Huyu kijana inaonesha kichwani fuse hazipo sawa sawa na Chadema wanamuangalia tuu.
 
Mdude ni kichaa...chadema waangalie jinsi ya kum-handle
 
Huyu kijana inaonesha kichwani fuse hazipo sawa sawa na Chadema wanamuangalia tuu.

Dhalimu wa Chattle mlimchukulia hatua gani kipindi anapora fedha za Bureau de change na korosho? Mnatuletea kilio kwa mambo mepesi wakati mlikalia kimya uovu wa yule kiongozi dhalimu?
 
Bananga anataka kusema Mdude alikuwa mgonjwa wa akili kabla hajapelekwa jela? au amekuwa mgonjwa wa akili baada ya kutoka jela?

Mdude jana hakumtukana Rais, ni kauli aliyoitoa ndio imeonekana kuwashangaza/shtua wengi, japo nina hakika wengi wenu mkiambiwa muoneshe tusi kwenye ile kauli hamtaweza, mnatumia hisia zaidi kuhukumu.

Mmekuwa mkifikiria hili jambo kwa upande mmoja tu, kwanini hamfikirii na mateso aliyopitia Mdude akiwa gerezani muda wote huo kwa makosa ya kubambikiwa?

Nae ni binadamu, ana hisia, muacheni atoe frustrations zake, badala ya kusema akajifungie ndani huku sheria za nchi zikiendelea kuvunjwa, na mvunjaji ndio mnamlinda kama malaika, mnamvimbisha kichwa azidi kujisahau aendelee kufanya apendavyo.

Ikulu ni ofisi ya umma, na yeyote anaekaa pale ana jukumu la kuwatumikia wananchi bila kujali itikadi zao, usawa na haki viwepo kwa wote, akijisahau kwa hilo ni lazima akumbushwe, mahaba yenu kwa "mama" yatazidi kumuharibu, amkeni.
Mdude asidhani atatujazia magereza tu......nadhani labda dola iangalie namna
 
Am speechless [emoji87]
Tulilia wengi alipoteseka gerezani
Tulihuzunika sana alipolazimishiwa makosa ya uongo ili apotezwe.
Tumepigana wengi Mdude chadema kuwa huru.
Alipotoka jela alistahili yafuatayo;

1-Akaione familia yake akae nayo kwa muda
2-Apata physician amfanyie check up ya afya yake kwa kina (muda aliokaa gerezani ni mwingi sana).
3-Apatikane psychologist akae nae kumjenga kisaikolojia ili akitoka kuingia kwenye harakati aingie akiwa imara kimwili, kiakili na kimaono.
.
Kuendelea kumpatia kipaza sauti mapema haya SIONI TUNACHOJENGA, SIONI TUKIMSAIDIA, SIONI TUKIMPENDA MDUDE!
.
Sio lazima mnielewe na sio lazima mfanye hili ila TUFIKIRIE MAUMIVU TULIYOPITIA KAMA TUNA UTAYARI WA KUYAPOKEA TENA.
.
Alitufunza Mkiti freeman mbowetz kwamba tuyakatae mauti, tuivuke mitego inayotegwa kwetu kuturudisha nyuma maana hakuna faida kufa ama kusota jela. Tutapoteza muda wa kujenga chama kwa ajili ya kupigania walio jela, tutapoteza rasilimali watu kama tutakufa, tazama leo hakuna Alphonce Mawazo tena. Tutampata wapi Mawazo? Familia yake itampata wapi mwingine?
.
Ni muda wa kufikiri aina ya harakati zetu towards...... Bora kuwa mkimbizi uanzishie mashambilizi ukiwa mahali ambapo hata mbu hakung'ati kuliko kujitoa muhanga hivi ukiwa huna uhakika wa KUSOMA ULICHOANDIKA!
.
Msimamo huu ni wangu, usipoupenda uheshimu wa kwako.
Mdude anafanywa mtaji wa kisiasa na wana chadema wenzake.

Lazima atumiwe yeye kwa sasa ili itafutwe sympathy kwa wananchi.

Lakini jambo zuri ni kuwa pengine hao wananchi wakaishia kumuonea huruma tu huyo mdude kama mwanachi mwenzao lakini wasivutike na atakayoyasema.

Mdude anapoteza muda wake tu.
 
Back
Top Bottom