Bananga anataka kusema Mdude alikuwa mgonjwa wa akili kabla hajapelekwa jela? au amekuwa mgonjwa wa akili baada ya kutoka jela?
Mdude jana hakumtukana Rais, ni kauli aliyoitoa ndio imeonekana kuwashangaza/shtua wengi, japo nina hakika wengi wenu mkiambiwa muoneshe tusi kwenye ile kauli hamtaweza, mnatumia hisia zaidi kuhukumu.
Mmekuwa mkifikiria hili jambo kwa upande mmoja tu, kwanini hamfikirii na mateso aliyopitia Mdude akiwa gerezani muda wote huo kwa makosa ya kubambikiwa?
Nae ni binadamu, ana hisia, muacheni atoe frustrations zake, badala ya kusema akajifungie ndani huku sheria za nchi zikiendelea kuvunjwa, na mvunjaji ndio mnamlinda kama malaika, mnamvimbisha kichwa azidi kujisahau aendelee kufanya apendavyo.
Ikulu ni ofisi ya umma, na yeyote anaekaa pale ana jukumu la kuwatumikia wananchi bila kujali itikadi zao, usawa na haki viwepo kwa wote, akijisahau kwa hilo ni lazima akumbushwe, mahaba yenu kwa "mama" yatazidi kumuharibu, amkeni.