LGE2024 Ally Hapi ahimiza Wananchi kujitokeza kupiga kura

LGE2024 Ally Hapi ahimiza Wananchi kujitokeza kupiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Ally Hapi, amehitimisha kampeni za chama hicho mkoani Mbeya kwa kuhimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024. Katika hotuba yake, Hapi alisisitiza umuhimu wa kampeni za kistaarabu zinazojikita katika kuhamasisha maendeleo badala ya siasa za chuki.

Alieleza kuwa CCM imejipambanua kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, na maji chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan

Soma Pia: Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024


Huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa na imani na viongozi wa CCM, akisema kwamba rekodi yao inaonyesha matokeo ya kweli na kujali maslahi ya wananchi.

Hapi pia alisisitiza kwamba wagombea wa CCM wana uwezo wa kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo na kuleta mabadiliko chanya kwa jamii, pamoja na kuhimiza wananchi kuchagua viongozi wenye sera na uwezo wa kuboresha maisha yao.
 
Back
Top Bottom