Kwa yaliyotokea 29/10, mtu yoyote, bila kujali chama ama historia yake ya nyuma, akijitokeza kulaani tena kwa vitendo na kuukana utawala wa Samia, kudai uchunguzi huru na adhabu kwa wauaji, anahitaji pongezi kubwa. Huyu ni binadamu aliyekamilika, mwenye utu, anayejali wenzake. Hili tu linatosha mimi binafsi kumsamehe Msigwa kwa yale aliyotenda na kusema. Kwa upande mwingine, wenye mashaka au chuki naye, nitawaelewa vile vile ila tujipe muda tuone mwisho wake.