Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Ali Hapi akizungumza katika hafla ya mapokezi ya wajumbe wa sekretarieti ya CCM amesema kuwa CCM imeingia kwenye mapambano, hivyo upinzani wasitegemee huruma.
"Naomba wakati huu ambao tunaingia kwenye mapambano niwaambie wale jamaa wa upande wa pili (vyama vya upinzani) ambao kazi yao ni kelele tu, Rais amewatengenezea mazingira mazuri wanafanya mikutano, wanafanya shughuli zao nyingine, wamepewa ruzuku lakini shukrani hawana, na niliwasikia wengine wanalalamika kwenye uchaguzi mdogo wanasema kwamba mbona hawajatuachia, yaani CCM ifanye kazi ya kuwaachia kata kweli?
Wasitegemee huruma uchaguzi ni kazi na malengo yetu ni kuendelea kushika dola, na sisi tuko tayari kuendelea kukiendesha chama chetu, muda wa kuoneana huruma umekwisha, mikutano wote tunafanya, kujipanga wote tunajipanga habari za kubebwa hazipo, twende kwa wananchi tukatafute kura, twende kwa wananchi tukarejeshe na kuongeza heshima ya ushindi wa CCM"