Pre GE2025 Ally Hapi: Vijana nguvu ya vyama vya Ukombozi, asisitiza uongozi imara

Pre GE2025 Ally Hapi: Vijana nguvu ya vyama vya Ukombozi, asisitiza uongozi imara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

upupu255

Senior Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
119
Reaction score
144
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Ally Hapi, amesema kuwa ili vyama sita vya siasa vilivyoshiriki harakati za ukombozi katika nchi za kusini mwa Afrika viendelee kuwa vyama vya watu, lazima viendelee kutoa fursa sawa na haki ndani ya vyama vyenyewe.

Amesema ni muhimu vyama vya siasa kuendelea kuwajengea uwezo vijana kwani hakuna chama kitakachoendelea bila kuwekeza kwa kundi hilo.

Hapi amesema hayo mjini Kibaha, akifunga mafunzo ya siku kumi kwa viongozi na wawakilishi kutoka vyama sita vilivyoshiriki harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika. Vyama hivyo ni ANC (Afrika Kusini), FRELIMO (Msumbiji), CCM (Tanzania), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia) na ZANU-PF (Zimbabwe). Mafunzo hayo yalifanyika kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere ya Kwamfipa.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Alisema kuwa ni lazima vijana waandaliwe na kupatiwa mafunzo ya itikadi, uzalendo, na wajue historia ya nchi zao. Vilevile, alisisitiza umuhimu wa kujifunza uvumilivu, akisema kwamba uongozi si jambo la kugombea tu, bali pia ni lazima kukubali changamoto na kushinda wakati wa vikwazo.

“Kwa hiyo, ili vyama viendelee kuwa na umoja, viungwe mkono na wananchi, lazima vyama viwe na taswira ya Umoja na mshikamano. CCM tayari imeonyesha uongozi katika eneo hili, na tumefanya hivyo kwa muda mrefu sana,” alisema Hapi.

Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Marcelina Chijoliga, alisema kuwa mafunzo hayo ya siku kumi yalikusudia kuwaandaa viongozi wa kisiasa na wananchi kwa mageuzi.

Alifafanua kuwa wahitimu 90 wanatarajiwa kuleta mageuzi kwa maisha ya wananchi, huku baadhi ya washiriki wakieleza kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kisiasa kutoka kwa nchi zao.

Walisisitiza kuwa wengi wanakabiliwa na changamoto ya uchumi wa Taifa, lakini walionyesha matumaini ya kuboresha hali ya kiuchumi kwa ushirikiano na uongozi bora.

 
Back
Top Bottom