Ally Kamwe msemaji wa Yanga afungwe break, Haya sasa Mzee wa watu kakujibu kiutu uzima

Ally Kamwe msemaji wa Yanga afungwe break, Haya sasa Mzee wa watu kakujibu kiutu uzima

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
1,484
Reaction score
2,852
BAADA YA KUDHIHAKIWA NA ALIKAMWE, JUMA MGUNDA AMPA JIBU

🗣️"Yanga ni Club yetu pekee Tanzania inayotuwakilisha kwenye fainaly hii ya CAF na kwa bahati iliyonjema inacheza na Club Inayotoka nje ya nchi yetu.

🗣️Sijui kinachopelekea mimi kuwa miongoni mwa kampeni hii ya matusi na kunidhalilisha Nilidhani kampeni itakuwa ni kushinda fainally, kuliko hiki alichokifanya Mwanangu Ally Kamwe.

🗣️Namuombea kwa Mungu awe na mwisho mzuri, mimi nimeshuhudia watu wengi wakifanya kazi Yanga na Simba na sasa wapo nje ya mfumo.

🗣️Kama nilipaswa kutukanwa ili Yanga ishinde basi nimekubali ili Taifa langu lijivunie .

🗣️Tusiposhinda kesho nitashangaa sana kwanini tumefungwa wakati kilichotakiwa kifanywe kimefanywa juu yangu na familia yangu" Kocha Juma Mgunda.

Akiwa ktk kampeni za mechi ya tarehe 28/05/2023 huko Zakhiem Mbagala aliwauliza mashaabiki kati ya "Mgunda na andazi" utachagua nini. Mashaabiki wakaitikia "andazi" . Hakutosheka akauliza tena"kati ya wasimamizi wa Feisal na andazi utachagua nini. Mashaabiki tena wakajibu "andazi".

Sasa mimi kama mtu mzima naona Ally Kamwe alichofanya ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa malezi na makuzi ya wazazi wake. Huwezi kumlinganisha mtu mzima mwenye umri sawa na baba yako na "andazi".

Mgunda amekuwa Hana utani wa Simba na Yanga hata ktk media sjawahi kumskia akitoa maneno ya shobo kwa Wana Yanga. Iweje leo mbele ya watu tena wa rika tofauti tofauti umlinganishe na andazi.

Haya sasa kakujibu kiutu uzima kama baba. Kazi kwako.
 
Katika hili, na nikiwa kama mshabiki wa Yanga; naungana na wadau wote wa michezo kukemea aina hii ya udhalilishaji. Ifikie wakati hawa wasemaji wa vilabu vya mpira nchini mwetu, waache kujigeuza kuwa waimba taarab.

Dogo anatakiwa kufahamu ya kwamba andazi linalinganishwa na ccm tu! Na siyo Juma Mgunda, kocha wa watu asiye na makuu! Au hata mtukutu wetu Fei Toto.
 
Alikosea na amekiri kukosea na kujutia. Ameomba radhi, hata kabla ya Mgunda kuzungumza.

Kila mtu anakosea, ila anayeomba radhi ni muungwana.

Japo kaomba kwenye page yake ya Instagram, angepaswa kwenda kuomba kwenye vyombo vya habari kwenye kadamnasi kama ya jana..

Binafsi kamaa mwanalunyasi, nimemsamehe. Mgunda pia, ni mtu muungwana sana. Atamsamehe.

Na zaidi, Mungu anajua. Kama kamaanisha basi naye amemsamehe.
 
[emoji2788]Kama nilipaswa kutukanwa ili Yanga ishinde basi nimekubali ili Taifa langu lijivunie .
Mgunda kaongea maneno mazito sana. Kwani Ali Kamwe alianza vipi hadi kufikia kwa Mgunda? Mbona mechi ni Yanga vs USM Alger na bora hata angekuwa kamtupia madongo Ahmed Ally tungesema labda karudisha madongo. Sasa huyu baba wa watu kamuanzia nini?
 
Katika hili, na nikiwa kama mshabiki wa Yanga; naungana na wadau wote wa michezo kukemea aina hii ya udhalilishaji. Ifikie hawa wasemaji wa vilabu waache kujigeuza kuwa waimba taarab.

Dogo anatakiwa kufahamu ya kwamba andazi linalinganishwa na ccm tu! Na siyo Juma Mgunda, kocha wa watu asiye na makuu! Au hata mtukutu wetu Fei Toto.
Yeap, hakupaswa kusema upumbavu wa namna hii, na Mzee Mgunda ametumia busara sana saana kujibu. Mungu ibariki Tanzania
 
Klabu ya yangu Yanga inatakiwa itoke hadharani imuombe radhi Mgunda. Maana kauli ya Ali Kamwe ni kauli ya Yanga. Kudhibiti mambo kama haya siku za mbeleni huyo mtu awajabishwe.

Nilidhani tumetoka zama za kina Jerry Muro na Manara kumbe bado.
 
BAADA YA KUDHIHAKIWA NA ALIKAMWE, JUMA MGUNDA AMPA JIBU

🗣️"Yanga ni Club yetu pekee Tanzania inayotuwakilisha kwenye fainaly hii ya CAF na kwa bahati iliyonjema inacheza na Club Inayotoka nje ya nchi yetu.

🗣️Sijui kinachopelekea mimi kuwa miongoni mwa kampeni hii ya matusi na kunidhalilisha Nilidhani kampeni itakuwa ni kushinda fainally , kuliko hiki alichokifanya Mwanangu Ally Kamwe.

🗣️Namuombea kwa Mungu awe na mwisho mzuri , mimi nimeshuhudia watu wengi wakifanya kazi Yanga na Simba na sasa wapo nje ya mfumo.

🗣️Kama nilipaswa kutukanwa ili Yanga ishinde basi nimekubali ili Taifa langu lijivunie .

🗣️Tusiposhinda kesho nitashangaa sana kwanini tumefungwa wakati kilichotakiwa kifanywe kimefanywa juu yangu na familia yangu" Kocha Juma Mgunda.

Akiwa ktk kampeni za mechi ya tarehe 28/05/2023 huko Zakhiem Mbagala aliwauliza mashaabiki kati ya "Mgunda na andazi" utachagua nini. Mashaabiki wakaitikia "andazi" . Hakutosheka akauliza tena"kati ya wasimamizi wa Feisal na andazi utachagua nini. Mashaabiki tena wakajibu "andazi".

Sasa mimi km mtu mzima naona Ally Kamwe alichofanya ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa malezi na makuzi ya wazazi wake. Huwezi kumlinganisha mtu mzima mwenye umri sawa na baba yako na "andazi". Mgunda amekuwa Hana utani wa Simba na Yanga hata ktk media sjawahi kumskia akitoa maneno ya shobo kwa Wana Yanga. Iweje leo mbele ya watu tena wa rika tofauti tofauti umlinganishe na andazi.

Haya sasa kakujibu kiutu uzima km baba. Kazi kwako.
Furaha ikizidi mipaka huharibu msingi
 
Aly ameomba radhi , amejua kama amekosea na atamuomba radhi kadri siku zinavyoenda mbele.

Lakini sasa ajenda itabadilika na kumshambulia Aly Kamwe .

Tunakula kakisea lakini kaomba asamehewe kuna binadamu ambaye hafanyi makosa?

Naomba Tu Kesho yanga tushinde kwa sababu tukifungwa watu wataanza kusema ni laana za Mgunda na Aly atakuwa kwenye kikaango kikubwa Sana.

Kila la kheri YANGA , Muungwana akivuliwa nguo huchutama Aly kachutama kesi iishe.
 
Katika hili, na nikiwa kama mshabiki wa Yanga; naungana na wadau wote wa michezo kukemea aina hii ya udhalilishaji. Ifikie wakati hawa wasemaji wa vilabu vya mpira nchini mwetu, waache kujigeuza kuwa waimba taarab.

Dogo anatakiwa kufahamu ya kwamba andazi linalinganishwa na ccm tu! Na siyo Juma Mgunda, kocha wa watu asiye na makuu! Au hata mtukutu wetu Fei Toto.
Hiki kitengo kimekosewa sawa kuwapa watoto wavulana, kilipaswa kipewe watu wazima ambao wana busara, hekima, na wanaojielewa. Sio hawa wavulana wanaondeshwa na mihemko na utoto mwingi.
 
Aly ameomba radhi , amejua kama amekosea na atamuomba radhi kadri siku zinavyoenda mbele.

Lakini sasa ajenda itabadilika na kumshambulia Aly Kamwe .

Tunakula kakisea lakini kaomba asamehewe kuna binadamu ambaye hafanyi makosa?

Naomba Tu Kesho yanga tushinde kwa sababu tukifungwa watu wataanza kusema ni laana za Mgunda na Aly atakuwa kwenye kikaango kikubwa Sana.

Kila la kheri YANGA , Muungwana akivuliwa nguo huchutama Aly kachutama kesi iishe.
Hili tatizo la uropokaji, waanzilishi wake ni Haji Manara na Jerry Muro. Na hawa vijana wawili (Ali Kamwe wa Yanga na Ahmed Ali wa simba) nao wanataka kufuata nyendo zao.

Hivyo ni vizuri wakajirekebisha mapema ili kuulinda mpira wetu wa miguu, usionekane ni kituko.
 
Pole kwa Mgunda na sisi Wana Timu ya Wananchi tunazidi kumuombea radhi Ally Kamwe.

Japo kwa hatua aliyokuwa amefikia alikuwa amejisahau yeye ni nani ndani ya Timu ya Wananchi na ndio hata kuna wakati alikuwa akiongea na waandishi ye anajibu tu kama mtu wa kijiweni na kuisahau nafasi yake.

Kwa alichokifanya jana ni dhahiri amepata cha kujifunza na siku nyingine hatofanya vitu kwa mihemko.
 
Alikosea na amekiri kukosea na kujutia. Ameomba radhi, hata kabla ya Mgunda kuzungumza.

Kila mtu anakosea, ila anayeomba radhi ni muungwana.

Japo kaomba kwenye page yake ya Instagram, angepaswa kwenda kuomba kwenye vyombo vya habari kwenye halaiki kama ya jana..

Binafsi kamaa mwanalunyasi, nimemsamehe. Mgunda pia, ni mtu muungwana sana. Atamsamehe.

Na zaidi, Mungu anajua. Kama kamaanisha basi naye amemsamehe.
Paragraph yako ya 3 aizingatie.

Mimi siyo shaabiki wa Team za NBC ila ninashaabikia mchezo wa mpira wa miguu,ni shaabiki wa Barcelona lkn kati ya vitu ambavyo kinakosewa Tz ni kwamba Team zetu hazijui kuwa anachokisema msemaji na ndio kauli ya team hivyo anapaswa kuzungumza kile alichoambiwa kusema.

Sasa hapa kwetu msemaji eti yupo kwa ajili ya kukera watu.
Yaani cheo cha msemaji wa team (mkurugenzi wa mawasiliano na habari)wa team hakina thamani kiasi cha kutoa matusi hovyohovyo na wa upande wake (team yake wanafurahia sana pale anapo kera watu) Nilitarajia kwa hatua walipofikia Young Africa waombe radhi kupitia ukurasa wao kwani huu ndio muda wa kuvuna wapenzi wenye akili timamu na wa kuwaunga mkono popote na nyakati zote.
 
Back
Top Bottom