Ally Kamwe msemaji wa Yanga afungwe break, Haya sasa Mzee wa watu kakujibu kiutu uzima

Ally Kamwe msemaji wa Yanga afungwe break, Haya sasa Mzee wa watu kakujibu kiutu uzima

BAADA YA KUDHIHAKIWA NA ALIKAMWE, JUMA MGUNDA AMPA JIBU

[emoji2788]"Yanga ni Club yetu pekee Tanzania inayotuwakilisha kwenye fainaly hii ya CAF na kwa bahati iliyonjema inacheza na Club Inayotoka nje ya nchi yetu.

[emoji2788]Sijui kinachopelekea mimi kuwa miongoni mwa kampeni hii ya matusi na kunidhalilisha Nilidhani kampeni itakuwa ni kushinda fainally, kuliko hiki alichokifanya Mwanangu Ally Kamwe.

[emoji2788]Namuombea kwa Mungu awe na mwisho mzuri, mimi nimeshuhudia watu wengi wakifanya kazi Yanga na Simba na sasa wapo nje ya mfumo.

[emoji2788]Kama nilipaswa kutukanwa ili Yanga ishinde basi nimekubali ili Taifa langu lijivunie .

[emoji2788]Tusiposhinda kesho nitashangaa sana kwanini tumefungwa wakati kilichotakiwa kifanywe kimefanywa juu yangu na familia yangu" Kocha Juma Mgunda.

Akiwa ktk kampeni za mechi ya tarehe 28/05/2023 huko Zakhiem Mbagala aliwauliza mashaabiki kati ya "Mgunda na andazi" utachagua nini. Mashaabiki wakaitikia "andazi" . Hakutosheka akauliza tena"kati ya wasimamizi wa Feisal na andazi utachagua nini. Mashaabiki tena wakajibu "andazi".

Sasa mimi kama mtu mzima naona Ally Kamwe alichofanya ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa malezi na makuzi ya wazazi wake. Huwezi kumlinganisha mtu mzima mwenye umri sawa na baba yako na "andazi".

Mgunda amekuwa Hana utani wa Simba na Yanga hata ktk media sjawahi kumskia akitoa maneno ya shobo kwa Wana Yanga. Iweje leo mbele ya watu tena wa rika tofauti tofauti umlinganishe na andazi.

Haya sasa kakujibu kiutu uzima kama baba. Kazi kwako.
Waaxhe upumbavu kuikuzs hii. Ukiwa katika hizi taasisi mbili unapaswa utegemee kila aina ya madongo.

Dejan, Rage, Ykipe, Mo dewji, Manar, Ahmed Ally, Babra na watu kibao wameshapigwa sana madongo katika hii tasnia.Why leo mgunda?

Utani wa jadi utabaki palepale.

NA MIMI NAKAZIA , KATI YA MGUNDA NA ANDAZI TUTACHAGUA ANDAZI..!
 
Muulize Manara atakuambia alivyopelekewa moto na Karia baada ya kuchutama.

Kuna muda namna nzuri ya kumfundisha mtu ni kupitia adhabu. Sio kila kichwa kina uwezo wa kujifunza kupitia msamaha. Ukifuatilia mfululizo wa matamshi ya huyo jamaa utagundua sio msamaha unaomfaa.
IMG-20230528-WA0043.jpg
 
Mimi najiuliza dogo alikuwa anatafuta nini? Mgunda ameingiaje?
Watoto wadogo wanapewa vyeo vinavyowazidi uwezo.
Mtoto ananuka maziwa ya mama yake anapewa majukumu mazito ambayo hajui hata mipaka yake.
Ukurugenzi wa habari katika club siyo madaraka madogo. Kuisemea club kunahitaji hekima, siyo kubwabwaja tu ili kuwafurahisha mashabiki.
 
Kwa hiyo wewe ulivyoambiwa ukachekea?

Inabidi uchunguzwe kama kichwani ni salama!!
Acha kuchukulia kila jambo kuwa halisi! Kwahiyo Roma akamatwe na CCM kisa kaimba andazi n Bora kuliko wao?.
 
Pole kwa Mgunda na sisi Wana Timu ya Wananchi tunazidi kumuombea radhi Ally Kamwe.

Japo kwa hatua aliyokuwa amefikia alikuwa amejisahau yeye ni nani ndani ya Timu ya Wananchi na ndio hata kuna wakati alikuwa akiongea na waandishi ye anajibu tu kama mtu wa kijiweni na kuisahau nafasi yake.

Kwa alichokifanya jana ni dhahiri amepata cha kujifunza na siku nyingine hatofanya vitu kwa mihemko.
Hana cha kujifunza yy alitoka hadhari mtaanzisha comedy show ya kutucheka simba watu wakakemea sana na bado anafanya upuuzi wake na anaemtuma ni hersi
 
Back
Top Bottom