Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Sioni haja ya kulalama rais kafanya makubwa tumwache na tumpe miaka mingine atuvushe,lawama za nini? Au tunataka rais mla rushwa kitu ambacho JPM kakikataa?
Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
JPM hajazuia rushwa, alichofanya ni kuminya uhuru wa vyombo vya habari ili visitangaze mambo ya rushwa. Lengo hasa ni kuhadaa umma kuwa hamna rushwa ili akae madarakani atakavyo. Hilo la yeye kutaka kukaa madarakani alianza toka alipoingia madarakani kwa kuwatuma kuna Nkamia. Hii kunajisi chaguzi za nchi hii, ni ili kupata watu watakaomuongezea muda wa kukaa madarakani zaidi ya muda wa sasa wa katiba. Ila mjue mnacheza mchezo bwana hatari ile mbaya. Mchelea mwana kulia ...