Ally Kiba ni Messi, Diamond Ronaldo

Ally Kiba ni Messi, Diamond Ronaldo

kuna uzi ukizisoma huwezi kupita kimyakimya hata kama huna neno basi utalitafuta ili mradi uwepo wako na kuukubali huo uzi uonekane....bab kubwa muanzisha uzi
 
Hebu nielimishe muziki wa Africa ni upi?

Mpaka sasa mimi nawatambuwa Dr Remmy na Tatunane band ndio wametuwakilisha kwenye matamasha makubwa.

Hapa nahitaji kuelimishwa na siyo ubishani na porojo.

Asanta.


ungeenda Basata ungepata elimu unayotafuta.....naona umeanza kubishana na channel O, infact kwenye list huwaoni kina koffi olomide wala awilo kwa sbabu list hii ni kwaajili ya wale wasanii waliobadilisha game ya afrika kutoka ndombolo ya solo(bolingo) kufikia hapo ilipo ndo maana unamuona Fally ipupa cuz yy ameimodernize bolingo..

we shikilia wakina doctor remy wako tu
 
Hebu nielimishe muziki wa Africa ni upi?

Mpaka sasa mimi nawatambuwa Dr Remmy na Tatunane band ndio wametuwakilisha kwenye matamasha makubwa.

Hapa nahitaji kuelimishwa na siyo ubishani na porojo.

Asanta.

Kawaulize channel O
Sisi vitendo tu
 
unajitahidi kuelezea ila naona una chuki kwa dimond sema unazificha kwenye maneno kwa kumapka mafuta kwa mgongo wa chupa..

unatoa critiscism za kipuuzi kuwa Dimond ameacha shoo za nyumbani za watanzania waliompandisha?? hivi nikuulize unajua p square wapo wapi sasa??? kama hujui basi wanaishi zao atlanta wamehama kabisa nyumbani kwao Nigeria na bado wanafanya kazi nzuri sembuse huyu Dimond ambaye yupo sinza hapo,,,..

Dimond kwa level yake aliyofikia hapaswi kurudi nyuma kung'ang'ania shoo za uchwara kama Fiesta na zingine zenye mtonyo mdogo kwa kigezo cha eti watanzania walimpandisha, ushauri wako umejaa mawazo ya kimaskini...ni lini hapa bongo kuna promoter alimpa dimond hela anazotaka akakataa kupiga shoo?? kama anapiga shoo hadi kwenye birthday ya K Lyn we ulitaka aje akuimbie chumbani kwako mdogomdgo ndo ufurahie.........acha ujinga bwana

Duuu kazi kweli kweli!

Mashabiki tuna michango sana kwenye kuanguka kwa wasanii wetu!

Huyu jamaa katoa analysis nzuri sana na tusipende sana thread za kusifia wasanii wetu hizi zinazo wakosoa ndizo nzuri na zina jenga zaidi!

Ndio maana kuna watu husema tumepewa masikio mawili na mdomo mmoja ili tusikilize sana kuliko kuongea!
 
Hii ni moja ya thread nzuri sana hapa zinazo wahusu Alikiba na Diamond!

Diamond na Alikiba kila mtu ana umuhimu wake kwenye huu muziki!

Hii thread ina faa kuwa sticky!
 
Jisifie wajua kupga vyenga wajua kuimba sana but mwisho wa siku who makes more money ndiyo habari maana hakuna anayeimba kufurahisha watu.
Kama hai-make ela basi hai-make sense (Fid Q).

Trust me sio kwamba diamond anatengeneza pesa kihivyo no bali zaidi ni maigizo yake anayotufanyia kujionesha ana pesa, shoo ya ujerumani mnajua alifanya kwa bei gani?? Haikuzid euro 2000, na ukwel ni kwamba amesahau kwamba "wadau wanapenda wakuone jinsi ulivyo yaani uishi Maisha ya uhalisia na sio ya Maigizo" (Fid Q)
 
Duuu kazi kweli kweli!

Mashabiki tuna michango sana kwenye kuanguka kwa wasanii wetu!

Huyu jamaa katoa analysis nzuri sana na tusipende sana thread za kusifia wasanii wetu hizi zinazo wakosoa ndizo nzuri na zina jenga zaidi!

Ndio maana kuna watu husema tumepewa masikio mawili na mdomo mmoja ili tusikilize sana kuliko kuongea!

Jamaa ni shabiki tu..read between the lines
 
Back
Top Bottom