Almanusura brother kunyimwa mke ukweni

Ishu siyo kupigwa goti ishu hapo ni hiyo kuvishana pete,hivi haya mambo ya kishenzi shenzi mmeyarithi kutoka wapi?

Unamvalisha pete ili iweje na kwa faida ipi?
Binafsi sikuwaga na Mambo ya mapete,mababu na mababa zetu wamezekeana bila hizo mambo ya kilimbukeni ya kimapete kumpa padri hela ama wauzaji,iweje mie ndie nitoke kwa nature.
Ndoa kiafrika tunaishi swafi Kama ambavyo baba wa babu waliishi miaka iyo zamani before ya mkoloni. Waafrika bana mtt akiongea English anajisifia anaona Kama amesomesha mno
 
Maana yake hasa ni nini hii....yan walikua wana test kama muoaji anakula "tope" maana unyevu wa chakula na mchuz wake si unatengeza tope tope hapo chini.
Sasa angekuka tu ooohh hapo wana piga tick [emoji23][emoji23][emoji23]
Sisi wenyewe hata hatuelewi, tulimuuliza kwetu tunafanya hivi??, Huo ndio mwanzo wa kupewa libwata
 
Nina mashaka mnoo na hichi ulichoandika kama ni kweli.

Unasema kwenye hiyo gari ya IST waliyokuja nayo waoaji hakukuwa na mwanaume hata mmoja, wote walikuwa wanawake. Sasa hata muoaji (mwanaume) hakuwepo au naye alikuwa ni mwanamke?

Unasema muoaji alikuwa mmasai, sasa tangu lini wamasai wakapeleka ukweni wanawake tupu kusindikiza mwanaume kuoa? Unazijua mila za kimasai?

Unasema mlipanga shughuli iwe saa saba mchana, lakini waoaji wakachelewa 'mnoo' na kuja saa 10jioni kiasi cha wajomba kula na kusema na kusepa zao kabla ya waoaji kufika. Hivi kwa sisi waafrika na katika uhalisia wake, huo uchelewaji ni kitu kipya au cha ajabu mnoo kiasi cha wenyeji kususa?

Unasema waoaji walikuja na gari ya IST ikiwa na hivi vitu:
-Wanawake tupu (sijui ni wangapi? Labda tuseme walikuwa watano)
-Gunia la viazi
-Mikungu ya ndizi mitatu
-Kiroba cha sukari
-Mchele kilo 50
-Dumu moja la mafuta ya kula
-Gunia la viazi
-Mfuko wa ngano
Katika hali ya kawaida hiyo gari isingeweza kupakia hizo vitu zote na kuenea. Huo ni mzigo wa kubebwa na pick up au Kirikuu.
 
Ahaha mkuu now days tumebebwa na upepo wa culture na traditions za kimagharibi kwa kiwango kikubwa sanaa
 
Mm nashangaaga hata hizi engagement, dume linapiga goti ! Naghafilika Sana , yeye (ke) ndo anatakiwa apige goti, ama la tusimame wote ,,,,
Dume linapiga goti alafu linaangua kilio balaa kama dokta kumbuka birthday ya mkewe alilia kama kafiwa na mama mzazi😂😂
 
Mm nashangaaga hata hizi engagement, dume linapiga goti ! Naghafilika Sana , yeye (ke) ndo anatakiwa apige goti, ama la tusimame wote ,,,,

Mwanamke aombe ndoa?
Yeye ndo akawe kichwa wakifika huko ndani, uanze kulia kulia
 
Ishu siyo kupigwa goti ishu hapo ni hiyo kuvishana pete,hivi haya mambo ya kishenzi shenzi mmeyarithi kutoka wapi?

Unamvalisha pete ili iweje na kwa faida ipi?
Acha ujinga ulioridhishwa kutoka kwa Mama Edson( Ellen white) Nabii mwongo .
Uliza kwa uzuri utelekezwa maana ya pete
 
Mwanamke aombe ndoa?
Yeye ndo akawe kichwa wakifika huko ndani, uanze kulia kulia
Kiafrika mwanamke kupiga goti wala sio ishu..ni ishara ya heshima na adabu ndivyo mama zetu wamekua wakifunzwa ndio maana ndoa zao zinabaki kuwa bora sana kuliko hizi na haki sawa
 
Dume linapiga goti alafu linaangua kilio balaa kama dokta kumbuka birthday ya mkewe alilia kama kafiwa na mama mzazi😂😂
Yule sio mwanaume braza.Hata muda wa kufuatilia vimeo kama vile huwa sinaga..wale special group.
 
Nakujibu kama ifuatavyo,wamasai wanamila wanatangulia wanawake ukeni kuangalia boma then baada ya miezi kadhaa wanatangulia wanaume wakiwa na muoaji mwenyewe,sehemu sisi tulipo na kwahao wanaume sio mbali wengine walitangulia kwa miguu,na kwenye ist walikaa watu wa 3 mama mkwe alikuwa dereva,dada mtu anayeoa,na shangazi mtu,mbele wamekaa wawili nyuma kakaa mmoja,then siti ikavunjwa wakapakiza vitu kwenye siti na kwenye but,
Wajomba waliondoka mapema kwakuwa wanaishi moshi vijijini kule usafiri unasumbua wa kupanda masama
 
heko kwa bro, mimi sipigi hata tukiwa peke yetu chumbani, yaani hata iweje
bora aende kwao
 
Mambo ya mila na desturi, ya kawaida Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…