Almas Kasongo: Bodi ya ligi itatoa adhabu kwa Maofisa Habari wa timu wanaochekesha na kushindwa kuzungumzia Mpira

Itakuwa vizuri, makelele na mambo ya kijinga jinga yamezidi
 
Aanze na manara aliyesema yeye ni bingwa wa propaganda
 
Hawa wazee wanatakiwa waondoshwe mmoja baada ya mwingine. Yani mwenyekiti wa bodi ya ligi hata hafananii
 
Huyo Kasongo bwege kweli.
 
NI Tanzania tu mtu kucheka kwenye Mpira unapangiwa. hivi utajuaje huyu ameongea neno la kuchekesha
 
Mbona hata kwenye nyumba zetu za ibada viongozi wetu wa dini huwa wanatuchekesha??
Mpira wa Tanzania ni siasa tu.
 
Ally Kamwe naye ana mdomo mchafu tena hana adabu kabisa kumbuka ishu yake na kumlinganisha na andazi. Kwa ujumla wote hao wanne uliowataja wabadilike utani uwepo lakini isifike kukashifiana.
 
Basi angewaambia wanaosikiliza wasicheke, Yani atathibitishaje kama aliezungumza alikuwa na lengo la kuchekesha au no msikilizaji tu kaamua kucheka? atapimaje hivyo vichekesho? Kasongo amsona wasemaji wanapata majina kuliko yeye na raisi wake
 
Yupo sawa kabisa.
 
Ally Kamwe naye ana mdomo mchafu tena hana adabu kabisa kumbuka ishu yake na kumlinganisha na andazi. Kwa ujumla wote hao wanne uliowataja wabadilike utani uwepo lakini isifike kukashifiana.
Nilikua nimesahau, kumbe naye ni mshenzi mshenzi.
 
Ni sawa kabisa kwa maana vitengo vilikuwa vimeingiliwa na waimba taarab kutwa nzima ni mipasho tu, badala ya kuongea kiuweledi unakuwa comedy si Bora ukaungane na wakina bambo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…