Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mkoani Tabora, Mhe. Aloyce Kwezi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Hassan Suluhu kwa kutoa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.162 kwa ajili ya ujenzi wa shule za Msingi 4 katika Jimbo la kaliua.
Mhe. Kwezi amezitaja Shule hizo kuwa ni pamoja na Shule ya Msingi Magere Usimba Milioni 347.5, Mpandamlowoka Milioni 561.1, Upele Igwisi Milioni 91 na Wachawaseme Milioni 163.
Mhe. Kwezi amesema Mhe. Rais amekuwa kiongozi anayewajali wananchi katika kuhakikisha wanapata huduma bora za kielimu kwa kuweka miundombinu ya madarasa na vyoo katika shule mbalimbali ambapo amesema wananchi wa Jimbo la kaliua wanamshukuru na wanamuombea afya njema ili aendelee kuwatumikia.
Mhe. Kwezi amethibitisha kuwa fedha hizo zimeingia tarehe 22 March 2023 na zimeleta chachu kubwa ya maendeleo katika sekta ya elimu kwani kuna madarasa ambayo yalishaanza kujengwa.