Aloyce Nyanda wa Star TV aachiwa na Polisi baada ya kushikiliwa kwa muda

Aloyce Nyanda wa Star TV aachiwa na Polisi baada ya kushikiliwa kwa muda

Pole sana Classmate wangu SAUT Mwanza Edwin Soko na darasa letu la BAMC 2006 - 2009 ukiwa unakaa Hodtels za Malimbe na Mimi Hostels za Nsumba kwa Kukamatwa kwa Mwenzetu ( Mwanahabari ) Aloyce Nyanda.

Nimezipokea Taarifa hizi kwa Masikitiko makubwa sana hasa nikiamini kuwa Aloyce ni Mtu wa Maadili, Mwerevu na Makini zaidi Kiutendaji.

Ninaungana na TEC 100% kwa Tamko.
ohh
 
Wabongo kwa kelele hatujambo, mtu anakoroma nyuma ya keyboard kwa ID feki akitegemea amzuie mwarabu asiwekeze.

Jikotekeni kama Kenya kama hamuwezi msipige kelele
Kwa hiyo wewe unakoroma kutoka nyuma ya trekta au?
 
Taarifa ya kushikikiwa kwa Mwandishi Aliyce Nyanda

Nimepokea simu nyingi toka kwa waandishi mbalimbali juu ya kutaka kujua kama mwenzetu Mwandishi Aloyce Nyanda anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mwanza.

Ukweli ni kuwa, mwandishi mwenzetu aliitwa na jeshi la polisi na kushikiliwa kwa muda mchache na kuandikishwa maelezo kwenye kituo cha polisi.

Taarifa za ndani zaidi ni kuwa alikuwa anatuhumiwa kwa matumizi ya mitandao ya kijamii.

Baada ya kuandika maelezo aliachiwa ili aendelee na majukumu yake.

Tunaendelea kufuatilia jambo ili kama lina vina saba vya kuminya uhuru wa habari na haki ya kujieleza na pia usalama wake.

Edwin Soko
22.08.2023
Nape anachekelea huko alipo
 
Nyanda amekuwa radical juu ya mkataba wa bandari na amekuwa akifanya juhudi za kutaka kuhoji wanaopinga mkataba huu. Msimamo wake haupendwi na watawala.
 
duuh imekuwaje tena? au naye kaonesha hautaki huu mkataba wetu? aangalie fyucha yake aachane na haya mambo yasijemkuta ya yule mwenzake wa itv akarudi kuulilia umma anashindwa kumudu familia yake baada ya kupoteza kazi.
 
Pole sana Classmate wangu SAUT Mwanza Edwin Soko na darasa letu la BAMC 2006 - 2009 ukiwa unakaa Hodtels za Malimbe na Mimi Hostels za Nsumba kwa Kukamatwa kwa Mwenzetu ( Mwanahabari ) Aloyce Nyanda.

Nimezipokea Taarifa hizi kwa Masikitiko makubwa sana hasa nikiamini kuwa Aloyce ni Mtu wa Maadili, Mwerevu na Makini zaidi Kiutendaji.

Ninaungana na TEC 100% kwa Tamko.
Ungesomaga m
Sheria na wew unasomaje mass communication mkuu
 
Back
Top Bottom