JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mwanariadha Alphonce Simbu alipotua Nchini akitokea Ufaransa alihojiwa na hii ni sehemu ya maelezo yake kuhusu sababu za yeye kutofanya vizuri na kushinda Medali kwenye Michezo ya Olimpiki 2024 Jijini Paris:
"Kwanza kabisa tulitakiwa tujijue njia ambazo tutatumia kukimbia hata miezi miwili kabla ili tuweze kuifanyia mazoezi, kuanzia hapo lakini tuliijua siku za karibuni kabla ya kuelekea Paris, hiyo ilikuwa changamoto kwetu.
“Mfano mimi nilikimbia sana katika mteleko, nilipofika kwenye kilima kukawa na ugumu kidogo.
“Tuliona njia hiyo katika mtandao tu, tulivyofika tuliangalia tu ilivyochorwa lakini hatukuwa na nafasi ya kwenda kuifanyia mazoezi.
“Unajua njia sio tu kuiangalia lakini lazima uifanyie mazoezi, usipofanya hivyo kuitumia inakuwa ngumu.”
Alipoulizwa maoni yake kuhusu Olipimiki kwa jumla na Tanzania inafeli wapi mesema “Tuwe na tabia ya kukuza Vijana tusiwe na tabia ya kusubiri watu wajitokeze wenyewe inatengeneza ‘gape’, mfano tukiwa na program ya kutafuta wachezaji hasa vijijini, unajua kuna wachezaji wengi wa riadha wapo vijijini.
"Tukiwa na tabia hiyo ya kutafuta watu na kuwatengeneza kutakuwa hakuna tena ile tabia ya Mtu akistaafu panapoa haitakuwepo.”