Alshabaab wavamia "bus" na kuuwa watu wengi huko Wajir, Kenya

Wewe NI mpumbav,hivi polisi akisindikiza Basi Halitarushiwa risasi!Shukuru Mungu haya hayajatokea hapa kwetu!
Tatizo lenu ninyi ni kujifanya wajuaji wakati hamjui kitu na hamna uwezo wowote ule. Hilo tatizo sisi tulikua nalo miaka mingi sana, tulipoanza kusindikiza magari kwa pamoja chini ya ulinzi mkali, majambazi yamekimbia. Mnapaswa kuja kujifunza kwanini tunaishi kwa amani wakati tunazungukwa na nchi zenye migogoro,, kama vile DRC, Burundi na Rwanda.
 
Hilo ndio tatizo lenu, kujipiga kifua wakati uwezo wenu ni mdogo sana. Hivi kwanini msisindikize hayo magari yanayokwenda katika maeneo hayo kama Tanzania tunavyosindikiza magari yanayokwenda mikoa inayopakana na Burundi?
Tukisindikiza wanaweka IED kwenye barabara. Gaidi ni Gaidi na huwezi mshinda ujanja isipokuwa kumpiga risasi mbele ya dunia nzima. Angalau atafanya mambo yake mbali na Nairobi. Anajua humu tunagandana na yeye. Huko kwa border ninapendekeza KDF ifanye doria kwenye border na ukuta ujengwe. Majizi yakose njia ya kuvuka border iliyo wazi.
 
Wewe NI mpumbav,hivi polisi akisindikiza Basi Halitarushiwa risasi!Shukuru Mungu haya hayajatokea hapa kwetu!
Mwambie huyo Mtanzania mwenzako asiyefahamu hata Marekani wameshindwa kumaliza ugaidi duniani Waafrika ndio tutaweza? Wiki iliyopita gaidi alidunga visu na kuua watu wawili UK. Jana gaidi aliua watu watatu Marekani kwa kuwafyatulia risasi katika military base. Gaidi wanavaa nguo za raia kwa hivyo huwezi kuwatambua. Ukinyang'anya raia bunduki, gaidi anatumia kisu. Ukinyang'anya raia visu gaidi anatumia gari kufyeka watu kama huko Niece, France. joto la jiwe anadhani yeye ni mtaalam wa jinsi ya kumaliza ugaidi bali hajui lolote.
 
Msumbiji naona ugaidi ikiwaandama lakini wewe ni kuponda tu wafu Kenya
 
Nimesoma sehemu kwamba Police 7 ni miongoni mwa waliouwawa!

Police 7 wanauwawa kwa mpigo Kama Raia..... Askari gani hao?
 
Wewe una matatizo. Usiwahi linganisha jambazi wa kawaida wa kubeba bunduki na gaidi wa kubeba bomb. Hayo magari hata yakijazwa polisi mia moja, likipita juu ya IED mnapoteza polisi wenu wote. Shukuru mungu mnadili na majambazi na sio magaidi. Sisi tumepoteza polisi wengi kwa njia ya IED hadi sasa baadhi ya polisi wanatumia armoured vehicles katika maeneo haya.
 
Mnapaswa kununua MAGARI ya doria yasiyopenya risasi wala kuharibiwa na IED, hayo ndio yatangulie mbele yafuatiwe na msululu wa MAGARI ya abiria, mwisho Kuwepo na MAGARI mengine yasiyopenya risasi na askari wa kutosha.
 
Mnapaswa kununua MAGARI ya doria yasiyopenya risasi wala kuharibiwa na IED, hayo ndio yatangulie mbele yafuatiwe na msululu wa MAGARI ya abiria, mwisho Kuwepo na MAGARI mengine yasiyopenya risasi na askari wa kutosha.
Tupe hiyo pesa ya kununua hayo magari. Pengine Tanzania mnachuna pesa kwenye miti.
 
Hili la kulinda MAGARI ya abiria ni rahisi sana na linawezekana, ibaki ule ugaidi wa kujitoa mhanga ambao ni mgumu kuudhibiti. Acheni ubishi haya mambo yanawezekana, mbona Nigeria wamedhibiti Boko Haram kuvamia shule na mabasi ya abiria, iweje ninyi mnashindwa?, acheni ubishi, mkisindikiza civilian vehicles mtadhibiti hilo tatizo, hiyo haina maana kwamba ugaidi utaisha, ila hilo tatizo la ugaidi wa kuteka civilian vehicles litapungua, kama lilivyoisha tatizo la kushambulia vyuo vya elimu ya juu.
 
Tupe hiyo pesa ya kununua hayo magari. Pengine Tanzania mnachuna pesa kwenye miti.
Biggest GDP, vipi mshindwe kupata $500,00 kwa ajili ya kuokoa maisha ya wakenya, hivi BBI hadi sasa imetumia kiasi gani?
 
Dah...poleni shemeji zetu....lakini kama hamuwawezi kwanini msikae mezani? Kuliko hivi mnavyopoteza uhai na pesa nyingi[emoji2960]
 
Poleni sana majirani zetu
 
Sio kweli, wanapigania madaraka kwa kutumia kigezo cha dini kupata kuungwa mkono, ni sawa kutumia ukabila ili kupata kuungwa mkono.
Ulishamsikia kiongozi wa Alshabaab alichokisema?

Anataka target yao ni kuwa Afrika mashariki iwe chini ya dola ya kiislam.
 
Inabidi muimarishe ulinzi zaidi katika mpaka wenu na Somalia. Wekeni kambi za jeshi huko.
 
Hii sio taarifa nzuri kutoka kwa majirani zetu, poleni sana katika hili
 
Unajua Magaidi ni Watu WAOGA SANA, na ndio maana wanavizia.

Wangekuwa si waoga basi watangaze vita vya moja kwa moja bila kuvizia wala kuficha nyuso zao.

Na je unafikiri ni kwanini hasa magaidi wanaishambulia zaidi Kenya? lile suala la ninyi kuweka wanajeshi Somalia sio sababu?
 
Walianza kutuvamia na kuteka watu nyara hata kabla ya sisi kuenda Somalia. Walikuwa pia wanateka watalii nyara. Hatungefumba macho na kujifanya kuwa wao ndio wanaume na sisi ni wanawake. Tuliamua kuingia Somalia na kupambana nao uso kwa uso macho kwa macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…