Aluta continua, Wakenya kesho kila mmoja paza sauti

Aluta continua, Wakenya kesho kila mmoja paza sauti

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Tujitokeze kuwapa vijana wetu nguvu, tujitahidi yawe maandamano ya amani ila polisi (FFU) wakiliamsha inabidi twende nao vivyo hivyo, uzuri kwenye hili tumeungana sote hamna migawanyiko, kimsingi ni serikali isikilize na kufanyia kazi malalamiko, wala hatuna ugomvi.

Wapambe wa rais mshaurini vizuri asichukulie poa, akubali kukutana na vijana wetu na kuskliza na kufanyia kazi malalamiko na baada ya hapo maisha yatarudia hali ya kawaida, ila mkimpa jeuri afanye ubabe, itabidi ngoma ichezwe usiku wote, wiki yote, je hawa polisi wamejiandaa vipi mikimbio ya kila siku.

Halafu kuna huyu dogo alichomoka nduki na farasi ya polisi, jameni aombwe airejeshe, ha ha ha hii nchi movie kila siku....
Bei Facebook anmelden
 
Aisei patamu.... mabomu ya machozi hayatoshi, leteni mengine, hongereni madogo, nenda mbele kwa mbele....
Huyu dogo hapa kaona isiwe tabu, amesimama juu ya lori la polisi

photo-protester.jpg
 
Hali tete, polisi wamezidiwa hadi inabidi wasaidiwe na vijana, wamefyatua mabomu hadi yanawatesa wenyewe....
Rais wetu kubali kuongea na hawa vijana, fahamu hawaendeshwi na mwanasiasa yeyote, wapo wenyewe kiuzalendo, utawaua lakini hautaweza kuua wote.

WhatsApp Image 2024-06-25 at 16.24.46_5883298d.jpg
 
Hali tete, polisi wamezidiwa hadi inabidi wasaidiwe na vijana, wamefyatua mabomu hadi yanawatesa wenyewe....
Rais wetu kubali kuongea na hawa vijana, fahamu hawaendeshwi na mwanasiasa yeyote, wapo wenyewe kiuzalendo, utawaua lakini hautaweza kuua wote.

View attachment 3025978
Subirieni usiku ruto anawafyatua....hamjui alikuwa na kesi ICC
 
Hali tete, polisi wamezidiwa hadi inabidi wasaidiwe na vijana, wamefyatua mabomu hadi yanawatesa wenyewe....
Rais wetu kubali kuongea na hawa vijana, fahamu hawaendeshwi na mwanasiasa yeyote, wapo wenyewe kiuzalendo, utawaua lakini hautaweza kuua wote.

View attachment 3025978
Anasaidiwa na waandamanaji?
Hao vijana hawana ubaya wowote. Ni wacha Mungu wanaoipenda nchi yao!
 
Back
Top Bottom