Hahahaha umenikumbusha mbali my dear lol, hapo pa kubembeleza wangu hasa ilikua kwenye kula nadhani pauline angeona usumbufu wa huyu ndio asingezaa kabisa mwe! mpaka ameze kijiko kimoja cha uji umeshajiimbisha, unaamka unamchezea na hata ngoma nidio anacheka uji unaenda unaanza tena kingine mpaka uishe viungo vyote vinauma aisee, yaani huyu mtoto alinifanya nikae nyumbani muda mrefu maana hakuna ambae alikua anamuweza kwenye kula, ila ukishamaliza hizo kero unasahau kabisa kesho unaanza tena lol, Mwenyezi Mungu alitupa ujasiri wa ajabu sana sisi wamama.
Ngoja nijipigie makofi he! na wamama wote popote mlipo kwa kwa kwa! maana kulea si mchezo ati