Kibu katukosesha goli la wazi Leo...
Tatizo lake anaambiwa kila siku na anashindwa kukaa chini na kufanyia kazi.
Kibu akifika golini yeye ni kuuputa mpira tu huku kafumba macho au anaangalia chini.
Kama anasoma humu aangalie goli la John Boko la tatu.
Boko kabla ya kupiga aliangalia goli, alimwangalia Golikipa akachagua pa kuupeleka mpira akafunga.
Angakuwa Kibu Di angauputa tu mpira na asingefunga, ama angamlenga kipa audake kama alivyofanya alipobaki yeye na kipa na akakosa, au angeupaisha.
KIBU DENNISI kabla ya kupiga mpira golini mwangalie golikipa, liangalie goli ndio ujue uupige wapi mpira wako.
Hivi huangalii video zako baada ya mchezo ?
Kwanini hujirekebishi ?
Goli ulilokosa Boko angafunga na uzee wake.
Chama anafunga mata nyingi tu.
Wewe ndio mshambuliaji kijana wa Simba na umri unakuruhusu, hujiulizi una magoli mangapi hadi sasa ?
Umekosa magoli mangapi na kwanini hasa.
Babu Boko angecheza mechi ulizocheza angakuwa na magoli mengi zaidi kwa sasa.
Kibu kama utaendelea hivyo hutaki kujirekebisha huu ni mkataba wako ni wa mwisho Simba.
Huna msaada kwa timu, hebu fanya mazoezi binafsi ya kufunga goli ili uache hizo papara zako
Hakuna mdau wa Simba anayefurahia jinsi unavyo ikosesha timu magoli mengi ya wazi kabisa.
Wanakushinda hata mabeki akina Kapombe na Shabalala kwa uwezo wa kufunga magoli...!
Hii ni aibu sana kwako Kibu.
Hebu toa hayo Marasta yako naona ukiwa uwanjani unafikiria jinsi ya kuzipanga nywele zako badala ya kuwa makini na majukumu yako.
Kibu huitendei haki Simba wala Wadau wa Simba waliokuamini na kukupa majukumu.
Fanya mazoezi binafsi ya kufunga usimtegemee kocha.
Akina Messi unaosikia wanafunga wanajifua sana na mazoezi Binafsi, Shabala, Kapombe na hata Chama wanafanya zana mazoezi Binafsi kwao ndio yanayo wafanya wawe bora.
Hakuna mshabiki wa Simba kwa sasa anakuwa na furaha akikuona umeanza First Eleven.
Hii ni changamoto kwako ya kuifanyia kazi haraka sana, la sivyo utakuja kupigwa na chupa za maji muda sio mrefu.
Nipo nimekaa hapa.