Ama watendaji dawasa wanamdharau waziri weso au waziri Aweso anafanya usanii kwa wananchi!

Ama watendaji dawasa wanamdharau waziri weso au waziri Aweso anafanya usanii kwa wananchi!

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
317
Reaction score
520
AMA WATENDAJI DAWASA WANAMDHARAU WAZIRI AWESO AU WAZIRI AWESO ANAFANYA USANII KWA WANANCHI!

WADAU poleni na majukumu ya mchana kutwa. Nataka kuzungumzia tatizo la maji maeneo ya Tabata, Kinyerezi, Bonyokwa na Kifuru.

Hivi karibuni, Waziri wa Maji, Juma Aweso alitembelea baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam ambayo yana matatizo ya upatikanaji wa maji.

Aliongea ya kuongea. Tena nakumbuka alimsimamisha kazi mtendaji mmoja kwa kile kilichoonekana kutowajibika sawasawa hadi wananchi wa maeneo hayo wakawa hawapati maji sawasawa.

Baada ya ziara ile, maji yalianza kupatikana ijapokuwa siyo kwa kiwango cha kumpigia makofi waziri.

Cha ajabu, sasa hivi katika maeneo hayo, ni wiki ya pili sasa maji hayatoki! Wanaouza maji ya visima wamepandisha bei (kufa kufaana).

Wananchi wanajiuliza tatizo liko wapi? Wengine wanasema watendaji wa Dawasa wanamdharau Waziri Aweso au Waziri Aweso na watendaji wake kuna wanalolijua lakini hawaliweki wazi.

Leo nimeleta kwa ufupi sana ili nione Waziri Aweso atachukua hatua gani? Ila zikipita siku tatu hakuna maji nitaanika madhaifu mengi ya Dawasa maeneo hato niliyokwisha kuyataja.

Angalizo: Pengine katika maeneo hayo kuna wanaopata maji. Basi hongera zao. Wengine maji hakuna.
 
Back
Top Bottom