SI KWELI PreGE2025 Amani Golugwa amesema CHADEMA imesitisha mikutano yote nchini hadi taarifa kamili itakapotolewa

SI KWELI PreGE2025 Amani Golugwa amesema CHADEMA imesitisha mikutano yote nchini hadi taarifa kamili itakapotolewa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wanabodi nimekutana na hii taarifa, Je, ni kweli CHADEMA wamesitisha mikutano yote nchini mpaka watakapotoa taarifa rasmi tena?
1744611554197.jpeg
1744611603028.jpeg
 
Tunachokijua
Amani Golugwa ni naibu Katibu Mkuu Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye aliteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho kutumikia nafasi hiyo, Tundu Lissu na kuthibitishwa na baraza kuu mnamo tarehe 22, Januari 2025.

Mnamo Mwezi April 11, 2025 Golugwa alifanya mkutano na waandishi wa wanahabari, makao makuu ya chama hicho Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Kutokana na mkutano huo kumeibuka taarifa zilizodaiwa kuchapishwa na Millard Ayo na Jambo Tv kuwa CHADEMA imesitisha mikutano yote nchini mpaka taarifa kamili itakapotolewa.


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu, (Key Word Search) umebaini kuwa Taarifa hiyo si ya kweli, kwani haijachapishwa kwenye kurasa za Millard Ayo na Jambo TV kama inavyoonekana katika grafiki hizo.

Vilevile machapisho hayo yamebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo uwepo wa mwezi Mei kwenye tarehe badala ya Aprili.

Aidha katika mkutano wake na waandishi wa habari wa Aprili 11, 2025 Golugwa hakutoa kauli yoyote ya kusitisha mikutano ya chama hicho nchini, bali alisisitiza kuendelea kufanyika kwa mikutano hiyo licha ya mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu kuwa rumande.

"Nipende kuwajulisha kwamba, oparesheni ya No Reforms, No Election itaendelea, leo saa nane na nusu sekretarieti ya chama taifa itakutana katika ofisi zetu za hapa Mikocheni kujadiliana na kupanga muendelezo wa oparesheni hii, tunajua Mwenyekiti bado yupo rumande lakini viongozi waliopo tukiongozwa na makamu mwenyekiti bara, John Heche na makamu mwenyekiti Zanzibar Said Mzee na wajumbe wa kamati kuu, Oparesheni itaendelea."

Tazama hapa kuanzia dakika ya 51 : 52 hadi 52:27

View: https://www.youtube.com/live/zkYXcNds1ZA?si=hj3zoc1h6XcwPcUD

Hata hivyo siku moja baadaye Chama hicho kiliendelea na mikutano yake ya hadhara ambapo makamu mwenyekiti wa chama hicho John Heche alifanya mkutano wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ikiwa ni muendelezo wa ratiba ya mikutano ya chama hicho.​
Back
Top Bottom