Amani Iliyofichwa na Ukimya wa hofu si ya kweli

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Kulikuwa na mji ambao wananchi wake walianza kudai haki zao. Walitaka huduma bora, usawa, na sauti yao isikike. Lakini badala ya kusikilizwa, wanasiasa walipanda majukwaani na kusema:

“Msilete fujo… amani ni bora kuliko yote.”

“Wanaodai haki si watu wa maendeleo… ni wavurugaji.”

“Hawa wanaopiga kelele hawapendi nchi yao.”

“Wananchi wema wananyamaza, wanakaa kwenye meza ya mazungumzo… si kama hawa wachache wenye chuki wanaotaka kutugawa.”

Wengine wakaanza kuogopa. Wengine wakaanza kunyamaza. Na wengine wakaanza kuamini kuwa kweli wanaodai haki ni tatizo.
Maneno hayo yaingiza sumu ya mgawanyiko baina ya watu wa maeneo hayo ikawa badhii wanasema

“Kama unadai haki sana, basi wewe si mmoja wetu.” “Unataka kutuletea shida, sisi tunataka amani.” Polepole, madai ya haki yakageuzwa kuwa kosa.
Ukweli ukaitwa uchochezi. Na ukimya ukaitwa amani.

Chuki ikaanza kukua kimya kimya, si kati ya viongozi tu, bali hata kwa wananchi wenyewe. Lakini ndani ya mioyo ya wengi, maumivu yaliongezeka.
Kwa sababu walijua hiyo haikuwa amani ya kweli…

Ilikuwa ni hofu na mgawanyiko uliovikwa jina la amani. Wakati huo huo, haki zao zilikuwa zinapotea kimyakimya.

Na wale waliothubutu kuzungumza, walitengwa, wakadhihakiwa, na kuitwa wabaya.
 
Naunga mkono hoja
P
 
Back
Top Bottom