Amani Manengelo, Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza, ameripotiwa kutekwa na kupotea tangu tarehe 14.02.2025 huko Misungwi, Mwanza.
Ameandika
Martin Maranja Masese
Amani Manengelo ni kiongozi wa vijana wa CHADEMA mkoa wa Mwanza. Katibu wa BAVICHA Mkoa - Mwanza.
Nimepata habari za kutekwa na kupotea Manengelo nimesikitika sana… kwamba vitendo hivi vinaendelea?
Inaelezwa kwamba, Amani Manengelo alitekwa na watu wasiojulikana siku ya 14.02.2025, Misungwi, Mwanza.
Ni nchi zenye tawala dhalimu za kidikteta neiyo zinaweza kuteka vijana wadogo ambao ni wapinzani wa Serikali.
Nafikiri, sasa ni muda wa kuonesha vitendo dhidi ya maneno. Tuwaoneshe watekaji sisi siyo kuku bandani.
Yaitishwe maandamano makubwa ya kushinikiza watu wote waliotekwa na kupotea, warejeshwe kwa haraka.
Vijana wa CHADEMA Mwanza, ni wakati wa kuonesha nguvu ya umma kushinikiza Manengelo apatikane.
Tusiwaache wahuni kuamua nani atekwe na kupotezwa. Kesho watamteka mwingine na kila kitu kitaendelea.
Tunao uongozi mpya wa chama, na umesisitiza wazi utapambana na vitendo vya utekaji, ni muda muafaka.
Kwa kuwa wanatekwa wenzetu, tuoneshe kwa vitendo vitendo vya utekaji ni ushenzi na ushamba usiokubalika.
Kataa utekaji. Kataa utekaji. Kataa utekaji.