Amani ya DRC na kesho ya usalama wa Tanzania

mwanamichakato

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2015
Posts
1,188
Reaction score
1,090
Mungu ibariki Afrika na watu wake..Mungu wabariki Viongozi wetu

Vita na mauaji vinaendelea Kivu ya Kaskazini,Maelfu ya raia wanauwa kila leo. Biashara na shughuli kuu zote zimedorora. Janga la kibinadamu siku si nyingi yamkini kukawa na mauaji ya haraiki. Waasi wenye nguvu wanapambana kuteka maeneo nyeti yenye utajiri mkubwa wa madini.

Makombora yanapigwa mpaka kwenye hifadhi za wakimbizi. Congo RDC inatafunwa na kumegwa..Wakongo wanalia na kusaga meno.

Tanzania sio kisiwa, Jirani zetu wapo kwenye hali ngumu sana. Tuendelee kulala, Tuendelee kuwa watazamaji. Tuendelee kukaa kimya..Tuendelee kuwa wapole.
 
UNASHAURI NINI?
Wakongomani wanapata shida sana kama raia wa kawaida,hususan wamama na watoto.
Kosa lao ni nchi yao kuwa na utajiri wa madini.
Utajiri umekuwa Laana kwa taifa hili lenye watu wengi wajinga wasio elewa maslahi ya watu wao.
Wachonganishi wanawaletea silaha ili wapigane na wao waendelee kuchota madini kwa bei ya kutupwa.
Kwenye migodi kazi inaendelea.
Mitaani vita inapigwa, na mabepari hawajali.
Nchu jirani Uganda ,Ruwanda na Burundi Tanzania, zinaruhusu mali kupita nchini mwao bila vizuizi, na Silaha kuingizwa bila vizuizi.

kwanini kongo haiwekewi Vikwazo vya Silaha?
Kwa nini Wakuu wa vikosi vya M23 na Banyamulenge na marebelwengine Kupatiwa rest Warant (RB) ya kimataifa?

NADHANI IKO NAMNA HAPA
 
Tutafute ufumbuzi wa kudumu wa hili tatizo ..Kukoseakana amani kwa mmoja wa mwanachama wa Jumuiya zetu ikiwamo SADC,EAC ni kukosekana amani kwetu..

Duniani tunapita..Tutende wema kwa wasio na hatia..Tutende wema kwa wanaoteseka
 
Tumeshawazuunguka mutu kati sasa ni KUWATWANGA tu No connection na sponsa wao ....atakaye piga kelele tunaanza naye ...ni Mbula ya Mabanga mfulululizo

Goma Kusini
Nimejisikia furaha, let us wipe out those bandits.
 
Nikiyatazama matatizo ya DRC nadhani tuko spin. Katika flying spin ni wakati ndege inapokuwa out of control na ndege inakwenda( mbio) kuigonga ardhi.
Hapa tunatoka kwa uchawi gani? Tukitazama upande wa adui,kufahamu nani anapigana na sisi,tunaona kwamba adui zetu ni ndugu zetu( baba mmoja,mama mmoja).
Hapa tunatoka kwa uchawi gani?
Bado yule Rishi Sunak anasema anataka kuwapeleka asylum seekers Ruanda. Na hiyo ni baada ya Putin kusema anataka kuwapeleka Wagner Kongo.

Tazama hii Baghavad Gita chapter one

Natamani kuwaona wale ambao wako tayari kuwatumikia na kuwatuliza Kaurava wenye nia mbaya kwa kukusanyika hapa kupigana vita.

Sanjaya akasema: Ewe Mfalme; Bwana Krishna, kama ilivyoombwa na Arjuna, aliweka gari bora zaidi kati ya magari yote katikati ya majeshi mawili yanayowakabili babu wa Arjuna, gwiji wake na Wafalme wengine wote; na akamwambia Arjuna: Tazama askari hawa waliokusanyika!

Arjuna aliona wajomba zake, babu, walimu, wajomba wa mama, kaka, wana, wajukuu, na wandugu wengine katika jeshi.

Shida ya Arjuna

Baada ya kuwaona baba-mkwe, masahaba, na jamaa zake wote wakiwa wamesimama kwenye safu za majeshi mawili, Arjuna aliingiwa na huruma nyingi na kusema maneno haya kwa huzuni: Ewe Krishna, nikiwaona jamaa zangu wamesimama kwa hamu ya kupigana, viungo vyangu. kushindwa na mdomo wangu ukauka. Mwili wangu unatetemeka na nywele zangu zimesimama.

Upinde hutoka mkononi mwangu, na ngozi yangu inawaka sana. Kichwa changu kinageuka, siwezi kusimama kwa utulivu, na O Krishna, naona ishara mbaya. Sioni faida ya kuwaua jamaa zangu vitani.

Sitaki ushindi, wala raha wala ufalme, Ee Krishna. Ni nini matumizi ya ufalme, au starehe, au hata maisha, O Krishna? Kwa sababu wale wote tunaowatakia ufalme, starehe, na anasa wamesimama hapa kwa ajili ya vita, wakiyatoa maisha yao.

Sipendi kuua walimu, wajomba, wana, babu, wajomba wa mama, baba-mkwe, wajukuu, mashemeji na jamaa wengine wanaokaribia kutuua, hata kwa uhuru wa ulimwengu tatu. , achilia mbali ufalme huu wa kidunia, Ee Krishna.

Ee Bwana Krishna, tutapata raha gani katika kuwaua ndugu binamu zetu? Tukiwaua wahalifu hawa tutapata dhambi tu.

Kwa hiyo, tusiwaue ndugu binamu zetu. Tunawezaje kuwa na furaha baada ya kuwaua jamaa zetu, O Krishna?

Ingawa wamepofushwa na uchoyo, na hawaoni ubaya katika uharibifu wa familia, au dhambi kwa kuwa wasaliti kwa marafiki. Kwa nini sisi, ambao tunaona uovu waziwazi katika uharibifu wa familia, tusifikirie juu ya kugeuka kutoka kwa dhambi hii, O Krishna?

Arjuna Anaelezea Uovu wa Vita

Tamaduni za milele za familia na kanuni za maadili zinaharibiwa na uharibifu wa familia. Na uasherati unatawala katika familia kutokana na uharibifu wa mila ya familia.

Na uasherati unapotawala, Ewe Krishna, wanawake wa familia huharibika; wakati wanawake wamepotoshwa, kizazi kisichohitajika huzaliwa.

Hii huleta familia na wauaji wa familia kuzimu, kwa sababu roho za mababu zao hushushwa hadhi wanaponyimwa sadaka za sherehe za upendo na heshima na kizazi kisichohitajika.

Sifa za milele za utaratibu wa kijamii na mila za familia za wale wanaoharibu familia zao zinaharibiwa na tendo la dhambi la uharamu.

Tumeambiwa, Ee Krishna, kwamba watu ambao mila zao za familia zimeharibiwa lazima wakae kuzimu kwa muda mrefu.

Ole! Tuko tayari kutenda dhambi kubwa kwa kujitahidi kuwaua jamaa zetu kwa sababu ya tamaa ya anasa za ufalme.

Ingekuwa afadhali zaidi kwangu ikiwa ndugu binamu wataniua kwa silaha zao vitani huku mimi sina silaha na bila kupinga.

Wakati Kwenda Inakuwa Mgumu, Hata Wagumu Wanaweza Kudanganyika

Sanjaya akasema: Baada ya kusema haya kwenye uwanja wa vita na kutupa upinde na mshale wake kando, Arjuna aliketi kwenye kiti cha gari huku akili yake ikiwa imezidiwa na huzuni.

Sura ya 2
Lazima tuache chuki turudishe amani.
Mtu akiongea kuhusu kuacha chuki anaambiwa kwamba amelewa Injili: anaulizwa,:"Unawezaje kuacha chuki katika mambo ya siasa?"
Lakini,tunakwenda wapi na hizi chuki?

Leo (Ijumaa) ulikuwepo mkutano mkubwa Kivu; makamanda wakuu wa Jeshi la South Africa,Tanzania,na Malawi,na makamanda wa Jeshi la Kongo wamemutana kuijadili strategy.
View: https://youtube.com/shorts/syzjwOm4tM8?si=RQ2KW53WZQimLqzH
 
Ni vizuri Jeshi letu la wananchi likafagia hawa waasi wa M23 maana ukweli wakifanikiwa Congo na kujijenga kuna siku watatest mitambo yao bongo na tutakuwa tumechelewa. Hilo halikwepeki maana Ukila nguruwe huwezi kuacha!!

Congo , Burundi na Rwanda zenye utulivu tunazihitaji sana kwa kupata ushuru wa mizigo yao bandarini , hata SGR tunajenga tule pesa zao, hivyo dawa ni kuua waasi wote wa Congo maana wanavuruga bizness zetu na maziwa makuu
 
Mungu ibariki Afrika na watu wake..Mungu wabariki Viongozi wetu

Vita na mauaji vinaendelea Kivu ya Kaskazini,Maelfu ya raia wanauwa kila leo. Biashara na shughuli kuu zote zimedorora. Janga la kibinadamu siku si nyingi yamkini kukawa na mauaji ya haraiki. Waasi wenye nguvu wanapambana kuteka maeneo nyeti yenye utajiri mkubwa wa madini.

Makombora yanapigwa mpaka kwenye hifadhi za wakimbizi. Congo RDC inatafunwa na kumegwa..Wakongo wanalia na kusaga meno.

Tanzania sio kisiwa, Jirani zetu wapo kwenye hali ngumu sana. Tuendelee kulala, Tuendelee kuwa watazamaji. Tuendelee kukaa kimya..Tuendelee kuwa wapole.
Mambo haya bhwanah!
Sasa unataka Tanzania ikafanye lipi la ziada, hukujuwa kuwa tunao vijana wetu huko. Unataka tukatangaze vita huko ndipo ujue tunajali hali ya DRC?
Hata siyo swala la kibiashara hata kidogo, ndio uwe msukumo wetu wa kusaidia kupatikana huko.

Ni hivi, serikali ya Congo ni lazima ionyeshe nia ya kumaliza ujinga huo unaoisumbua miaka yote. Ni wacongo wenyewe, siyo sisi wanaotakiwa kutoa jasho na damu kuikomboa nchi yao. Sisi tutatoa msaada tu, kusaidia juhudi zao. Mgogoro kamwe hauwezi kuwa wetu.

Hatujaanza leo kuwasaidia majirani zetu, historia yetu inafahamika na yeyote katika hili,; lakini hatuendi Congo kununua mgogoro uwe mgogoro wetu.

Na kama msaada unahitajika kuwabana hawa wachokozi toka nje ya Congo wanaoulea mgogoro huo, tuwe tayari kukabili hilo. Lakini la ndani ya Congo, tuwape nguvu na ushirikiano waCongo wayamalize wenyewe.
 
Tumeshawazuunguka mutu kati sasa ni KUWATWANGA tu No connection na sponsa wao ....atakaye piga kelele tunaanza naye ...ni Mbula ya Mabanga mfulululizo

Goma Kusini
Nategemea unajuwa unachozungumza hapa, na siyo bla bla za kawaida.
 
Ukiangalia siku ya sherehe ya muungano rais wa congo alikaa pembeni ya rais na hata Yale maonesho ya makomando yanatuma salamu nzuri sana Kwa waasi

Ni kama jk alivyompiga biti paka kwa kupitia maonesho ya sherehe za muungano

Naona mama Naye ameamua kutuma salam Kwa njia hiyo Ili kama watajifanya hawaelewi basi kikosi kianze kazi yake pasipo kulaumiwa
 
Mambo haya bhwanah!
Sasa unataka Tanzania ikafanye lipi la ziada, hukujuwa kuwa tunao vijana wetu huko. Unataka tukatangaze vita huko ndipo ujue tunajali hali ya DRC?
Hata siyo swala la kibiashara hata kidogo, ndio uwe msukumo wetu wa kusaidia kupatikana huko.

Ni hivi, serikali ya Congo ni lazima ionyeshe nia ya kumaliza ujinga huo unaoisumbua miaka yote. Ni wacongo wenyewe, siyo sisi wanaotakiwa kutoa jasho na damu kuikomboa nchi yao. Sisi tutatoa msaada tu, kusaidia juhudi zao. Mgogoro kamwe hauwezi kuwa wetu.

Hatujaanza leo kuwasaidia majirani zetu, historia yetu inafahamika na yeyote katika hili,; lakini hatuendi Congo kununua mgogoro uwe mgogoro wetu.

Na kama msaada unahitajika kuwabana hawa wachokozi toka nje ya Congo wanaoulea mgogoro huo, tuwe tayari kukabili hilo. Lakini la ndani ya Congo, tuwape nguvu na ushirikiano waCongo wayamalize wenyewe.
Nafikiri Ile harufu/hali Udini iliyoingia kwenye vita vya DRC .ndiyo inaifanya Tanzania ilichukulie hili suala Kwa tahadhari kubwa! Sisi tupo vulnerable na delicate sana na Udini.Hali hii ni sawa na ya Msumbiji. ..
Maoni yangu!
 
Mungu ibariki Afrika na watu wake..Mungu wabariki Viongozi wetu

Vita na mauaji vinaendelea Kivu ya Kaskazini,Maelfu ya raia wanauwa kila leo. Biashara na shughuli kuu zote zimedorora. Janga la kibinadamu siku si nyingi yamkini kukawa na mauaji ya haraiki. Waasi wenye nguvu wanapambana kuteka maeneo nyeti yenye utajiri mkubwa wa madini.

Makombora yanapigwa mpaka kwenye hifadhi za wakimbizi. Congo RDC inatafunwa na kumegwa..Wakongo wanalia na kusaga meno.

Tanzania sio kisiwa, Jirani zetu wapo kwenye hali ngumu sana. Tuendelee kulala, Tuendelee kuwa watazamaji. Tuendelee kukaa kimya..Tuendelee kuwa wapole.
Kitupenkee tz inachoweza kwa sasa ni kupambana na chadema,nakuwapa waarabu njia za uchumi.
 
Ni vizuri Jeshi letu la wananchi likafagia hawa waasi wa M23 maana ukweli wakifanikiwa Congo na kujijenga kuna siku watatest mitambo yao bongo na tutakuwa tumechelewa. Hilo halikwepeki maana Ukila nguruwe huwezi kuacha!!

Congo , Burundi na Rwanda zenye utulivu tunazihitaji sana kwa kupata ushuru wa mizigo yao bandarini , hata SGR tunajenga tule pesa zao, hivyo dawa ni kuua waasi wote wa Congo maana wanavuruga bizness zetu na maziwa makuu
Na tumeanza ujenzi wa bandari yetu ndani ya congo ili kuvusha mizigo kutoka bandari ya Kalema Mpanda...hivyo nilazima Congo
iwe tulivu kwa gharama zozote zile na soon Tunakwenda kutoa FUNDISHO
 
Nafikiri Ile harufu/hali Udini iliyoingia kwenye vita vya DRC .ndiyo inaifanya Tanzania ilichukulie hili suala Kwa tahadhari kubwa! Sisi tupo vulnerable na delicate sana na Udini.Hali hii ni sawa na ya Msumbiji. ..
Maoni yangu!
DRC machafuko yao ni ya udini? M23 wanapigania dini gani huko? Ungesema ya ukabila ningekubaliana na wewe.

Mambo ya DRC na Msumbiji ni tofauti kabisa. Hakuna uhusiano wowote kati yake.
 
Mambo haya bhwanah!
Sasa unataka Tanzania ikafanye lipi la ziada, hukujuwa kuwa tunao vijana wetu huko. Unataka tukatangaze vita huko ndipo ujue tunajali hali ya DRC?
Hata siyo swala la kibiashara hata kidogo, ndio uwe msukumo wetu wa kusaidia kupatikana huko.

Ni hivi, serikali ya Congo ni lazima ionyeshe nia ya kumaliza ujinga huo unaoisumbua miaka yote. Ni wacongo wenyewe, siyo sisi wanaotakiwa kutoa jasho na damu kuikomboa nchi yao. Sisi tutatoa msaada tu, kusaidia juhudi zao. Mgogoro kamwe hauwezi kuwa wetu.

Hatujaanza leo kuwasaidia majirani zetu, historia yetu inafahamika na yeyote katika hili,; lakini hatuendi Congo kununua mgogoro uwe mgogoro wetu.

Na kama msaada unahitajika kuwabana hawa wachokozi toka nje ya Congo wanaoulea mgogoro huo, tuwe tayari kukabili hilo. Lakini la ndani ya Congo, tuwape nguvu na ushirikiano waCongo wayamalize wenyewe.

..SADC ya sasa hivi ina viongozi legelege.

..miaka ya 90 SADC ilisimama kidete dhidi ya wavamizi wa DRC na hilo likasaidia serikali isipinduliwe.

..DRC inateseka kwasababu wanachama wenzake ktk SADC hawajasimama pamoja na kukataa kwa maneno na matendo uamuzi dhidi ya mwanachama mwenzao.
 
Vita ya congo itamalizwa na wacongo wenyewe.Tanzania kimbelembele Cha Nini kuwapeleka wanajeshi kuuliwa congo.Ya nyumbani yamewashinda,mumeuza bandari zetu zote,mmefukuza watu wetu kule ngorongoro na kuwamilikisha waarabu,pesa za umma mnacheze mtakavyo yaani ya nyumbani yamewashinda lakini mnaenda kutatua ya jirani?
 
DRC machafuko yao ni ya udini? M23 wanapigania dini gani huko? Ungesema ya ukabila ningekubaliana na wewe.

Mambo ya DRC na Msumbiji ni tofauti kabisa. Hakuna uhusiano wowote kati yake.
Fuatilia haya mambo mkuu...ADF.waliwahi kusema wenyewe kuwa wanampigania Allah kule Congo, na wanasaidiwa n IS.

...mgogoro wa Congo ni complex ,hebu kasome habari za ADF wanachokifanya kule Beni .Jana tu wamechinja watu Kituo Cha Afya!
 
..SADC ya sasa hivi ina viongozi legelege.

..miaka ya 90 SADC ilisimama kidete dhidi ya wavamizi wa DRC na hilo likasaidia serikali isipinduliwe.

..DRC inateseka kwasababu wanachama wenzake ktk SADC hawajasimama pamoja na kukataa kwa maneno na matendo uamuzi dhidi ya mwanachama mwenzao.
Bila shaka unawazungumzia Zmbabwe na Angola waliokataa upumbavu.

Hata 2012, chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa; 'of all people', Kikwete aliwasambaratisha M23 wakakimbilia kwa wafadhiri wao Uganda na Rwanda, wakaenda kujiimarisha zaidi; na sasa kurudi kama walivyo rudi.

Inatakiwa wakati huu wakichapwa wasipewe nafasi ya kwenda kujificha huko kwa wanaowalea.

SADC wakati huu ni Africa Kusini, Tanzania na Malawi. Kuna mashaka sana kama vijana wetu wamepewa amri ya kufanya kazi kama ile waliyokuwa nayo chini ya UN (MONUSC). Mikutano ya Makamba na Kagame itakuwa imeondoa ari ya kuwachapa M23 kisawasawa. Hii inaweza kuhatarisha usalama wa vijana wenyewe, kama tulivyo shudia karibuni wakitwangwa kombora.
 
Fuatilia haya mambo mkuu...ADF.waliwahi kusema wenyewe kuwa wanampigania Allah kule Congo, na wanasaidiwa n IS.

...mgogoro wa Congo ni complex ,hebu kasome habari za ADF wanachokifanya kule Beni .Jana tu wamechinja watu Kituo Cha Afya!
Kwa sehemu kubwa swala siyo ADF sana, labda utake kuhamisha 'focus' tu toka kwa tatizo kubwa la M23 kwa sababu uzijuazo mwenyewe.
ADF ni tatizo si kwa DRC pekee, ni tatizo hasa la Uganda.
Hakuna nchi jirani zinazowasaidia ADF kuvuruga DRC, kama wanavyopewa msaada hao M23, ambao ni tatizo kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom