PreGE2025 Amani ya Taifa ni Kipaumbele – Tuikatae Siasa za Vuguvugu na Uchochezi

PreGE2025 Amani ya Taifa ni Kipaumbele – Tuikatae Siasa za Vuguvugu na Uchochezi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Katika kipindi hiki ambacho Tanzania inapiga hatua kubwa katika kuimarisha demokrasia na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya wanasiasa wakichagua njia za uchochezi na kuvuruga amani kwa maslahi binafsi ya kisiasa. Kauli na mienendo ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu katika siku za hivi karibuni zimeonesha wazi dhamira ya kutaka kuharibu utulivu wa taifa letu kwa kuhamasisha maandamano na kususia uchaguzi – jambo ambalo si tu linakiuka misingi ya kidemokrasia bali pia linawanyima Watanzania haki yao halali ya kushiriki katika mchakato wa kisiasa.

Katika kila taifa linalothamini demokrasia, uchaguzi huru na wa haki ndio njia sahihi ya kushindana kisiasa. Kususia uchaguzi au kujaribu kuuvuruga kupitia miito ya maandamano ni kujaribu kuzima sauti ya wananchi, ambao kwa mujibu wa Katiba, wana haki ya kuchagua viongozi wanaowataka kupitia sanduku la kura. Kitendo cha Mheshimiwa Lissu kupinga uchaguzi na kupandikiza chuki miongoni mwa wananchi kinaonesha kuwa lengo lake si kushindana kwa hoja bali kuleta taharuki na mtafaruku wa kisiasa.

Kwa upande mwingine, hatuwezi kupuuza kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa kwa njia ya amani, ustaarabu na maendeleo ya kweli. Uongozi wake umeleta mabadiliko chanya katika sekta mbalimbali ikiwemo diplomasia, uwekezaji, elimu, afya na uhuru wa kujieleza. Chini ya utawala wake, Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine za Afrika kwa jinsi inavyosimamia demokrasia na mazungumzo ya kisiasa kwa njia ya amani.

Iwapo kweli vyama vya upinzani vinataka kushindana kwa dhati, basi njia pekee na sahihi ni kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Huo ndio uwanja halali wa kisiasa. Kushiriki uchaguzi ni kuonesha heshima kwa wananchi, kwa Katiba ya nchi, na kwa misingi ya demokrasia ambayo wanadai kuilinda. Wito wa kuhamasisha vuguvugu na migomo siyo tu kwamba ni hatari kwa mustakabali wa nchi, bali pia unahatarisha maisha ya watu wasio na hatia wanaoweza kujikuta katikati ya machafuko yasiyo na maana.

Tanzania ni nchi ya amani, mshikamano na utulivu. Tusikubali kurudishwa nyuma na siasa za mihemko, uchochezi na ubinafsi. Tumuunge mkono Rais Samia katika juhudi zake za kujenga taifa lenye haki, umoja na maendeleo. Vyama vya siasa viwe sehemu ya mchakato wa kuijenga Tanzania kwa kushiriki uchaguzi, si kwa kuitumbukiza kwenye migogoro isiyo ya lazima.

Amani ni msingi wa maendeleo – tuilinde kwa gharama yoyote.
Hamna mtu ambae hapendi amani, lakini amani iendane na haki, amani ambayo haina mazingira ya usawa ni smoke screens
 
Taratibu za uchaguzi Tanzania ni uhaini tosha! Zinachochea uasi. Nasikitika kuona miaka yote hii hatujafanya uasi dhidi ya taratibu hizo.
 
Wewe Mapete unakuja kwa jina la kike ili kumtetea Kibibi jitu siyo? Tanganyika siyo Uarabuni ambako mna roho za kishetani na kuua ni kama kunywa maji.
We taahira mtavunjwa viuno amani yetu ni tunu yetu tutailinda kwa gharama yoyote, washenzy mnatumiwa km vibaraka
 
We taahira mtavunjwa viuno amani yetu ni tunu yetu tutailinda kwa gharama yoyote, washenzy mnatumiwa km vibaraka
Wewe Mapete unakuja kwa jina la kike ili kumtetea Kibibi jitu siyo? Tanganyika siyo Uarabuni ambako mna roho za kishetani na kuua ni kama kunywa maji.
 
Alichotenda ni uhaini, yeye ni mwanasheria na analijua hilo
Kuna vifungu na condition za kuitwa uhaini. Case ya lissu doesnt fit
From namna amekamatwa . Watu wa sheria wako hapa, and some of us tunazajua hizo condition sababu tume serve huko before
 
Tanzania inahitaji GEN Z wakali zaidi ya Kenya. Kuna ushamba mkubwa sana katika utawala
 
Back
Top Bottom