Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,104
- 5,659
Jana nimemsikiliza Happiness Magese Clouds TV, anadai anafanya awareness ya tatizo la uzazi ambalo amekumbana nalo yeye binafsi, anadai anafanya hivyo kwa sababu anaamini wamama wengi wa kiafrica wanasumbuliwa na tatizo hilo.
Happiness alikwenda mbali na kudai kwamba aina hiyo ya tatizo ambalo kwake lilibainika huko Africa Kusini ndio kwanza madaktrari wetu pale Muhimbili wanajifunza, sikuelewa wanajifunza ili kuwa aware au wanajifunza namna ya kutoa tiba.
Mimi kama Mzazi niliguswa sana na kipindi kile, maelezo yake pamoja na ya mtangazaji, sikumbi jina la ugonjwa lakini mjadala wao ulipanuka na kuwa wa kijamii zaidi, lilienda mpaka kwenye maswala ya vidonge vya uzazi wa Mpango, ambapo ndugu mtangazaji alielezea juu ya malalamiko ya mwanamama kutoka Morogoro aliyedai kwamba vidonge hivyo vimemzuru,
mwanamama huyo alikuwa analalamika kwamba Promotion ya vidonge hivyo ambayo ilikuwa imetoka kufanywa na Flora Mbasha inapotosha watu, sababu yeye Binafsi vidonge hivyo vimemzuru. Spora, mtangazaji wa kipindi hicho akadai yeye binafsi alipomuuliza flora juu ya madhara ya dawa hizo alisema haelewi kama zina madhara yeye alikuwa anafanya promotion tu.
Hoja ya dada Magese ilikuwa kwamba, vidonge hivyo vinaweza kupunguza uwezekano wa kupata tatizo la namna hiyo, na kuhusu madhara ya vidonge hivyo alicounter kwa kudai kila kitu kina madhara, akajaribu kuelezea namna condom zisivyo na tija katika kumkinga mwanamke n.k
Kwa kifupi, tatizo husika litampelekea Happiness asiweze kuzaa mtoto maishani mwake.
Sasa basi, wakati namshauri Happiness aliwasilishe tatizo lake kwa Mwenyezi Mungu, akamlilie na kuzungumza nae, ni kivipi amemtengeneza Mwanamke alafu ashindwe kupata mtoto? Lakini ajiandae kwa majidiliano Mazito na Mungu wake, naamini kwa wingi wa wema wake na mapenzi yake kwetu waja wake, Mwenyezi Mungu atampatia sio tu mtoto bali watoto kwa zaidi ya haja za moyo wake.
Hoja yangu ni Kwamba, Katika Mjadala husika, kitu ambacho hakikusemwa ama kwa bahati mbaya au kwa makusudi ni Kwamba, moja ya chanzo kikubwa sana cha wanawake wa kizazi hiki kushindwa kupata watoto ni MATOKEO YA MIMBA NYINGI SANA WALIZOTOA HUKO NYUMA.
KUMBUKUMBU
Happiness binafsi alisema amekuwa akipata mimba lakini zinaharibika.
Tuseme Ukweli kuokoa jamii yetu.