Ambao hatujawahi kunywa pombe au kuvuta sigara, tukutane hapa

Ambao hatujawahi kunywa pombe au kuvuta sigara, tukutane hapa

Cgara ambayo inawashwa mbele na nyuma mkuu na inachanganyiwaa Kwenye kutoa kitu Cha arushaaa kuletaa testa flaniiii mkuu pindi unavuta[emoji23][emoji23][emoji23]
Hizi bangi mnazovuta mnachanganya na sigara kali ni za wap wakuu?
 
Situmii hivyo vitu, na sina mpango wa kuja kuvitumia. Nilishawahi onja pombe mara Moja, ila matokeo hayakuwa mazuri. Nikajiapia sitopata niiguse tena.

Upande wa sigara, kipindi nipo chalii tulikuwa na mtindo wa kusokota gazeti alafu tunavuta kama sigara. Mara nyingi tulifanya hivyo tukiwa shule na watoto wengine. Sasa kuna jumapili moja niko home, nikiwa jikoni nikasokota karatasi langu na kuvuta, mshua akaniona. Alinipiga makofi kadhaa ya haraka haraka, alafu pale jikoni kulikuwa na kinu Cha wastani hivi akakichukua na kunivisha kichwani.

Sharti ikawa sitakiwi kukivua kile kinu hata pawe na sababu gani. Uzuri nilikuwa nishakunywa chai tayari, ila siku hiyo mchana sikuweza kula, maana ilikuwa nikajaribu kula kile kinu kinanizidia uzito. Na nikikiangusha tu, nachezea wakofi yasiyo na idadi Wala mpangilio. Mwisho wa siku nikaamua kutulia tu. Mshua yupo kwenye kiti anasoma gazeti, Mimi nimekaa pembeni yake huku nimeshikilia kinu. Akitaka kitu ndani alikuwa hanitumi, ananyuka kufata mwenyewe na Mimi ananiambia nimfate, hivyo nazunguka tu na kinu changu.

Muda huo bi mkubwa kaenda church, lakini hadi muda ambao kawaida huwa anarudi, siku hiyo hakurudi, sijui hata alipitia wapi. Nakumbuka nilikivaa kile kinu tokea kwenye mida ya saa tatu asubuhi hivi mpaka kwenye saa nane au tisa mchana, na hapo ni baada ya a bi mkubwa kurudi. Kile kinu kilikuwa kimetoka kutwangia kisamvu, nilivyokivua nilikuwa nahisi harufu ya kisamvu kwenye Kila kitu kinachopita karibu yangu.

Mpaka leo hii tukiongelea sigara popote lazima niikumbuke Ile siku.
Dingi yako alikua mkatili
 
Mimi nimetumia Bangi,sigara,pombe
Nashukuru nlifanikiwa kuacha.Japo na jilaumu sana kwanini nlitumia haya mataka taka.Sasa naishi vizuri maisha ya furaha na pesa ina jaa kila kukicha.
Kwamba hivyo vitu ndio vilichangia kukuchelewesha kufanikiwa ?
 
NB;

Hatujawai kuishi trust me...

Hujawai kua mwanaume

Trust me [emoji120][emoji120][emoji120]

Mimi nimekullia familia ya uchumi wa Kati way back huko....

Mimi ni handsome japo age lime enda ukiniona Kwa sura first time unajua kua this guy is innocent people...

Ndio Mungu aliniumba ivyo
Ulitaka kusemaje?
 
Ningekuwa sinywi pombe sijui ningekuwa nafanya nini kustarehe,

Nahisi nijgekuwa naboreka sana.
Nina mshikaji wangu yupo vizur kiuchumi sasa hatumii kilevi chochote,yeye akitoka kwenye mishughuliko yake muda wote yupo nyumban,huwa nahisi bado hajayaishi haya maisha....
 
Back
Top Bottom