Ambao Hatusherekei Siku ya kuzaliwa(Birthday)

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,303
Reaction score
23,064
Wakuu, sijui ni mimi mshamba au uhafidhina unanisumbua.
Yani kwanza naona ambao husherekea sikukuu hasa wanaume ni kama walaini vile au hujifanya maisha ya kizunguu.

Kwanza siku yenyewe ya kuzaliwa huwa inapita bila hata kushtuka, nikija kukumbuka labda nikute mtu kaweka status, na inaweza pita mwezi ndo nakuja shtuka imepitiliza.

Najiuliza sijui ni mimi tu au kuna wadau kama mimi?

General Mangi
 
Yaani kama mimi, huwa sinaga hata habari labda mchuchu wangu anikumbushe. Sasa mtiti unatokeaga nikisahau siku yake ya kuzaliwa huwa hapakaliki. Huwa najiuliza kama yangu hata sikumbuki je nitakumbuka ya mwenzangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu mm hata kwenye grup la clas ikitokea mtu anasherekea huwa simpongezi
 
Sijawahi kufikiria

Sent from my iPhone6 using JamiiForums mobile app
 
isitoshe unakuwa umezungukwa na wadau wa kike na kiume wanakuimbia huku unelifungua domo unasubiri kulishwa keki hepibesdei tuyuuu!
hepibesdei tuyuuu!
auoda yuu na!

hapana aisee..
hahahaa
 
Utumwa uliogangamala na kuota mizizi.

Kuiga kila kitu na kuuleta katika tamaduni zetu na kutegemea matokeo yale yale ni kujitoa ufahamu mchana kweupe.

Chochote kisicho na mizizi ya nyumbani ni vigumu sana kuniingia akilini mwangu.

Hivi ule wimbo unaoimbwa siku ya kuiadhimisha hii siku ya kuzaliwa kwa kiswahili unaimbwaje vile?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…