Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

Ambao mna marafiki huwa mnawapataje?

Mi naona kama ndio yatakayonikuta mbeleni.

Napenda urafiki ila urafiki siuwezi.
Huwa nakuaga rafiki wa faida sana ila sasa unakuta mwenzangu nikimchunguza naona kama shobo zimezidi upande wangu.

Na hakuna kitu sikipendi kama kuwa faida anapata yeye/wao mimi faida sipati

Kingine watu wakikujua jua sana nalo ni tatizo! Heshima inaoungua sana
Kinachobaki unakua tu na wale watu ambao unafahamiana nao ila siku likikukuta jambo kwakweli hamna wa kukukimbilia.

Najiona ntakavyokua kama FINCH
 
Me na wewe same same,naeza kuingia huko kwa group nikawa bubu. Hao wa zamani nao kila maisha yametutenganisha mnoo wengine sijui hata walipo. Yaani kupata rafiki mkashibana ni mtihani kweli kweli sijui hata nifanyeje [emoji26]
Kuna mdada huwa napenda ile life style, weekends hupost status wapo kwenye coaster wanaenda kutembelea yatima yani wanavibe hao, usiku wapo pengine wanamwagilia moyo....napenda kwakweli ila mi sina
 
Mi naona kama ndio yatakayonikuta mbeleni.
Napenda urafiki ila urafiki siuwezi.
Huwa nakuaga rafiki wa faida sana ila sasa unakuta mwenzangu nikimchunguza naona kama shobo zimezidi upande wangu.
Na hakuna kitu sikipendi kama kuwa faida anapata yeye/wao mimi faida sipati
Kingine watu wakikujua jua sana nalo ni tatizo! Heshima inaoungua sana
Kinachobaki unakua tu na wale watu ambao unafahamiana nao ila siku likikukuta jambo kwakweli hamna wa kukukimbilia.

Najiona ntakavyokua kama FINCH
Yani inakua ule urafiki wa vitu vya maana sio kuvaa vijora sare kwenda kupiga umbea kwa mtu 😂😂😂
 
Na mi nlikua hivo mtaa nlokua nakaa sikuwai kua na rafiki hata mmoja. Ofisini nlikua nao wawili na hao wawili mmoja nlisoma nae chuo basi. Nnakoishi sasa kuna kikundi nimejiunga cha kusaidiana kwenye shida na raha. Tunapeana mawazo mbali mbali ya kiuchumi basi siku zinaenda. Lakini humo kwenye kikundi pia sina rafiki. So unaweza ukajiunga tu kwenye vikundi mbali mbali kupata wa kuzikana ambao si lazima wawe marafiki.
 
Kosa lako linaanzia hapo unaposema unataka "marafiki wa faida"

Au labda mimi sikuelewi unachomaanisha, nilivokuelewa ni kuwa unataka kuwa na marafiki, ili upate faida hasa hasa ya kipesa, kama ni hivyo, iyo ni moja ya sababu ndo maana hupati marafiki. Sijui baadhi ya watu mkoje.

Ondoa hiyo mentality ovu ya kishetani, ya kujenga urafiki na mtu ili ufaidike na kitu fulani toka kwake, jenga urafiki na mtu kwa sababu mko compatible na mna enjoy each other's time.

Ndo maana baadhi ya matajiri hawataki urafiki na maskini, sababu wanawakwepa nyie Mnaotafuta marafiki wa faida, maana anajua umejenga naye mazoea sababu ya pesa zake, Na si kwasababu umependa uwepo wake Evelyn Salt
 
Kwakweli muda unavyozidi kusonga ugumu wa kuwa na rafiki ndio unaongezeka, maana wale mliosoma wote wengi wanakuwa wametawanyika sehemu mbalimbali wapo bize na majukumu na familia.

Makazini pia inategemea, kama ni sehemu umehamia hujaanzia hapo inakuwa vigumu kuwa na mazoea sana, inakuwa ni ule urafiki wa kwenda lunch pamoja ila nje ya kazi hamna urafiki wala kujuliana hali.

Tatizo hasa linawapata watu ambao ni introvert hii ni changamoto sana, inafika weekend unakosa hata wa kwenda kupata nae moja mbili kubadili mawazo.

Hii ni moja ya matokeo ya utandawazi na ukuaji wa social media, zamani urafiki uliwepo sababu ya kutembeleana kwasasa kila kitu kinaishia kwenye whatsapp na magroup ya mtandao.

Ni muhimu kupeana mbinu za kupata marafiki wa kweli maana ukiwa na shuhuli ndio unaona umuhimu wa marafiki na jamaa.
 
Kosa lako linaanzia hapo unaposema unataka "marafiki wa faida"

Au labda mimi sikuelewi unachomaanisha, nilivokuelewa ni kuwa unataka kuwa na marafiki, ili upate faida hasa hasa ya kipesa, kama ni hivyo, iyo ni moja ya sababu ndo maana hupati marafiki. Sijui baadhi ya watu mkoje.

Ondoa hiyo mentality ovu ya kishetani, ya kujenga urafiki na mtu ili ufaidike na kitu fulani toka kwake, jenga urafiki na mtu kwa sababu mko compatible na mna enjoy each other's time.

Ndo maana baadhi ya matajiri hawataki urafiki na maskini, sababu wanawakwepa nyie Mnaotafuta marafiki wa faida, maana anajua umejenga naye mazoea sababu ya pesa zake, Na si kwasababu umependa uwepo wake Evelyn Salt
Mungu akusamehe my dear nami nshakusamehe pia
 
Good morning jf....

Kuna hili swala nimekua nikijiuliza hivi karibuni, baada ya kuona sasa uzee umeanza kupiga hodi. Najiona umri umetangulia mbele halafu maisha ni kama nayaacha nyuma, ni kama naishi tofauti na umri wangu. Nimesogea umri wa kuozesha, kuondokewa na wapendwa (waliozeeka) na kukutana na mambo mengi ambayo nadhani yanahitaji watu....ila bahati mbaya sasa hao watu ndio sina.

Natamani kuwa na marafiki kuwa na watu, watu wa faida, watu ambao wanaweza kushare ramani za maisha, watu ambao tunaweza kupanga safari kwenda vituo vya wahitaji tukawape misaada, watu ambao nikihitaji kumwagilia moyo najua wapo, watu ambao nikikwama najua watakuwepo, kina mama wenzangu huwa wana vyama umuhimu wa vyama naujua ila mi hata chama sijawahi kuwa nacho....naishi mwenyewe mwenyewe tu hadi nawaza si nitakosa wa kunizika mie mwisho nizikwe na manispaa.

Wenye marafiki mnawapataje???
Tunawapata kwa kutumia pesa tuu hakuna kingine!
 
Back
Top Bottom