Kipunga
JF-Expert Member
- Mar 8, 2021
- 264
- 590
Wazee shkamoni vijana mambo vp naomba moja kwa moja niende kwenye mada.
Sitasahau nilivyopewa kesi ya wizi pale ccm kilumba Mwanza wakati wa kuaga mwili wa mzee magufuli ilikua hivi.
Siku hio nimefika uwanjani mapema mida ya saa1 za asubui nikakaguliwa kama kawaida nikaingia ndani basi nikatafta sehemu ya kukaa nikakaa nilikua mwenyewe tu.
Basi tumekaa pale mida ya saa nne mwili wa magu ukawa umewasili vilio vikatawala hadi wengine kuzimia.utaratibu yakuaga ukaanza viongozi wakawa wanaaga walipomaliza mc akatangaza kwamba wananchi hawataweza kuaga kama walivyo aga watu wa dar es laam akasema mwili utazungushwa mara tano pale uwanjani.
Basi jukwaa nililo kuwepo watu wakapaniki sana na wengine waka anza kushuka basi na nikaanza kushuka kufika kwenye geti la jukwa nikakuta kuna vurugu sana watu wanataka kushuka.
Na mim nikajipenyeza hadi katkat nikawa nimesimama nyuma ya mzee wa makamo pia ni shomeshombe wa kiarabu.
Kama dakika mbili hivi nikaona yule mzee kageuka na kujishika mifukoni palepale akasema kijana naomba pesa zangu na simu
Sijakaa sawa mzee kanikwida anasema umeniibia kijana naomba pesa zangu. Nikamwambia mzee mim sijaiba hata unisaki mzee anasema utawataja wenzio tuu bac muda ule geti likafunguliwa watu wakatawanyika mzee kanipeleka kwa mwnajeshi.
Mjeda akaskiliza akasema nenda kwa huyo.mzee akanivuta hadi kwa polisi akamwambia huyu ni mwizi ameniibia palepale nikaambiw kaa chini askari wanazidi kuongezeka pale mmoja akanizaba kibao cha shavu.
Wakamuuliza mzee una usafiri! Mzee akasema ee nina gari basi nikapigwa pingu nishikwa mkubeto hadi nje ya uwanja yule mzee alikua na gari aina ya hilux nyeupe nikaingizwa ndani ya gari hadi central police Mwanza nikawekwa ndani.
kufupisha story yule mzee tumemlipa milioni 3 na polisi laki1 hapa ninapoongea ndio nimetoka kama wiki moja sasa.
Lengo la uzi huu na wewe naomba usimulie kitu ambacho huta sahau asanteni bandugu.