Ndiomana neema ya Yesu ikaingilia kati..huwezi kuwa mkamilifu huwezi fata sheria zote mana ukikosa kwa moja umekosa kwa zote..ndio mana nasema waislamu hawana tumaini zaidi ya kushika sheria ambapo kimsingi ni ngumu kushika sheria ili kuupata ukamilifu..mwanadamu ni mdhaifu kuangukia dhambini ni kugusa tu.
#MaendeleoHayanaChama
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kazi ya neema ni kutukataza dhambi , maana hatutamuona Mungu pasipokuwa wakamilifu
Tito 2:11
Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;
Tito 2:12
nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa;
1 Petro 1:14
Kama watoto wa kutii msijifananishe na tamaa zenu za kwanza za ujinga wenu;
1 Petro 1:15
bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
1 Petro 1:16
kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
1 Petro 1:17
Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.
1 Petro 1:18
Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;
1 Petro 1:19
bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.