Ambaye ameweza kugundua Purpose ya maisha yake!! Aniambie alifanyaje fanyaje

Ambaye ameweza kugundua Purpose ya maisha yake!! Aniambie alifanyaje fanyaje

Kwa yote unayosema mimi nimeyafanya tangu nikiwa na miaka 20
Leo nakaribia kustaafu nikiwa na maisha mema kabisa

Nimebarikiwa kuwa katika nchi zisizo na bughudha na usumbufu wa aina yoyote, na hii inakufanya uishi bila wasiwasi wala woga

Kama husumbuliwi na makodi na kusimamishwa bila sababu, chuki za kijinga kwa watu, mambo hayaendi bila kutoa rushwa basi mambo yatakuwa mazuri tu

Ila katika yote uliyoyaandika nimeyaishi na mpaka sasa nayaishi maisha hayo kwa furaha sana

Kuamua kukata ticket ya ndege na kwenda kupumzika weekend tu hata iwe 2m tsh nakata naenda nakula nalala narudi

Kwa kweli Mungu ni mwema na umri wote sina maradhi kabisa na hili ndio muhimu, huwa nasikia tu kwa watu
Ila sio la kujisifia bali nililitambua zamani sana kwa kutokumtegemea binadamu bali kufanya kazi kwa bidii na kutunza hela
Sijawahi kuomba msaada kwa mtu maishani na sijawahi kulala njaa hata siku moja labda nijitakie kutokula

Namshukuru Mungu kila siku
70 inanukia haiko mbali labda nitafika nikiwa na afya njema
Sema Amiin
 
Kuna watu hawataelewa…..kama ni mmoja wapo basi Jitulize!

Kugundua purpose ya maisha yako ( purpose of your life) si kitu kidogo. Watu wanaweza kuishi maisha yao yote pasipo kujua. Binafsi bado sijagundua au sijawa na uhakika pamoja nimejaribu kusoma article mbali mbali.

Pindi ukijua utaonesha dalili zifuatazo

1. Unajisikia vizuri kimwili na kiakili (si rahisi kuugua)

2. Unajisikia raha kuamka asubuhi na mapema na kuanza siku mpya

3. Hakuna changamoto ya kukukatisha tamaa , Unafurahi kupambana na changamoto

4. Mtu mwenye tumaini kubwa hata kama unapitia magumu vipi

5. Unapenda na kufanya vitu vya maana vinavoleta tija kwene maisha

6. Kutambua Talanta zako na kuzitumia kuleta mabadiliko duniani

7. Pesa kwako si kipaumbele kwene kufanya vitu.

8. Hujilazimishi kufanya vitu vilivyo kwene malengo yako

9. Fursa na bahati nasibu zinaanza kujitokeza

10. Hujiona mwene nia na nguvu ya kufanya vitu vitokee
11.

Nk….
Kama umeshagundua tuambie uligunduaje na ulichukua muda gani!
Ni kwa Neema na Baraka za Mungu tunaishi kwa kuinjoy zawadi ya uhai, afya ya mwili na Roho. Mengine ni ziada kadiri ya karama, utashi bidii na mararifa ambayo pia ni zawadi kutoka kwa Mungu na kila moja wetu amepewa bure 🐒

Tumia vizuri vipawa alivyokujaalia Mungu, na daima uwe mwepesi kuskia sauti ya wito wa Mungu katika maisha yako. Na hapo utagundua purpose of your life 🐒

Maisha unayoishi ni sauti uliyoiskia na kuifuata. Nasasa hapo ikiwa imefuata sauti ya giza au nuru, the test of it ndiyo purpose of your life, and it's up on you to change it 🐒
 
DR Mambo Jambo Lete neno mkubwaz kwa upande wangu energy yangu I'me rudi
Hongera Sana Mkuu But Ili kugundua purpose sio kazi ya Siku Moja ni kazi ya Miezi even Miaka bils kufanya Ordeals zozote..

Yaani bila Kuchezea Energy na kufanya Meditation za Kutosha wengi hawafiki kwa sababu ni kazi ya Kujitoa na Ukubwa wa Willpower Ya kuifanya..

Wengine waliamua kuwa Monks Kabisa ili kuifanya kazi vizuri
 
Sijawahi kuomba msaada kwa mtu maishani
Baba yako ni msaada wako pekee labda km sio Baba yako basi Mama yako maana wao ndio wamefanikisha umefika ulipofika ukubari au ukatae itabaki kua hivyo kwa hio usiseme 'sijawahi kuomba msaada kwa mtu' hao wazazi wako 'mama ataka kunya' unasubiri uvuliwe nguo ili unye ujisaidie hujasaidiwa hapo?

Hapo bado kuna ndugu, Jamaa na marafiki, coworkers na wengineo wengi waliokusaidia, wanaokusaidia na wanaoendelea kukusaidia kwa miaka mingi invisibly wengine mpaka kuchangia sherehe zako zote ulizowahi kuzifanya wamekuchangia means wamekusaidia yaan wanakusaidia bila wewe kuwaona kwa hio usiseme kwamba ooh maishani sijawahi kumuomba mtu msaada, yaan temamate chini
 
Baba yako ni msaada wako pekee labda km sio Baba yako basi Mama yako maana wao ndio wamefanikisha umefika ulipofika ukubari au ukatae itabaki kua hivyo kwa hio usiseme 'sijawahi kuomba msaada kwa mtu' hao wazazi wako 'mama ataka kunya' unasubiri uvuliwe nguo ili unye ujisaidie hujasaidiwa hapo?

Hapo bado kuna ndugu, Jamaa na marafiki wanaokusaidia invisibly yaan wanakusaidia bila wewe kuwaona kwa hio usiseme kwamba ooh maishani sijawahi kumuomba mtu msaada, yaan temamate

Baba yako ni msaada wako pekee labda km sio Baba yako basi Mama yako maana wao ndio wamefanikisha umefika ulipofika ukubari au ukatae itabaki kua hivyo kwa hio usiseme 'sijawahi kuomba msaada kwa mtu' hao wazazi wako 'mama ataka kunya' unasubiri uvuliwe nguo ili unye ujisaidie hujasaidiwa hapo?

Hapo bado kuna ndugu, Jamaa na marafiki wanaokusaidia invisibly yaan wanakusaidia bila wewe kuwaona kwa hio usiseme kwamba ooh maishani sijawahi kumuomba mtu msaada, yaan temamate chini
Mkuu kuomba na kusaidiwa ni mambo mawili tofauti kabisa
Asiesaidiwa na wazazi ni yatima tu aliepoteza wazazi akiwa mdogo

Wazazi wangu wamenilea mpaka nilipofika 18 na ninawashukuru mpaka kufa
Baada ya kuondoka nyumbani nilijitegemea mwenyewe na kuishi mbali na home kwa miaka isiyopungua 50
Siwezi kukufuru kama unavyodhani na mwenye wazazi hawezi kuacha kuwashukuru
Hata ticket ya ndege ya kwanza walinikatia wao

Siwezi hata siku moja kuacha kuwaombea kwa Mungu
Kusema niko mbali na nyumbani miaka yote hiyo maana yake nilikuwa najitegemea mwenyewe huku na Mungu ni mwema kila wakati sithubutu kukufuru
 
Asiesaidiwa na wazazi ni yatima tu aliepoteza wazazi akiwa mdogo
Maana yake uliposema 'maishani mwangu sijawahi kuomba mtu msaada' ulikua haupo sahihi mwenyewe umekubari kwamba umewakosea mpaka wazazi wako kwa kusema hukuwahi kuwaomba msaada hata wa kukuzaa ukimaanisha ungetangulia ungewazaa wewe? Kiburi cha Pesa na mafanikio unaona kilivyolevya Nafsi yako

Wewe umesaidiwa sana mpaka ulipofika iwe kwa kuomba au kwa kutokuomba Ila ulipofika ni kwa sababu ya misaada ya watu awe boss wako awe mkeo awe Mchungaji awe Baba Paroko awe Shekhe awe Imamu
 
Labda nitie neno kidogo Kwa sehemu juu ya kile ninachokijua au kuexperience

Purpose/Kusudi ni jambo la muhimu Sana Kwa mwanadamu yoyote kulifahamu na Kwa muktadha huo kama hulijui Kusudi la kuwepo kwako kuishi kwako ni sawa na kupoteza muda.

Naweza nisieleweke kidgo ila kadri ninavyoandika utaelewa najaribu kukusemesha kitu Gani.

Sijajua Kwa upande wa dini nyingine ila Kwa wakristo inaaminika kuwa kabla mwanadamu hajaumbwa duniani yaani wewe au Mimi kuwepo kwetu duniani lilianza kufikiriwa Kusudi kwanza Kisha nkaletwa au nkazaliwa ili nilitimize hilo Kusudi

Kwa namna nyepesi kuishi njenya Hilo ni kupoteza muda
Kupitia kitabu Cha Yeremia hayo yanabainishwa

=>Yeremia 1:5
Yeremia 1:
(Jeremiah)

5. Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
"Before I formed you in the womb I knew you; Before you were born I sanctified you; I ordained you a prophet to the nations."

Unaona kipi kimetangulia Sasa vuta picha Mungu amemuandaa Yeremia kuja kuwa Nabii Halaf yeye baada ya kuja duniani asitambue Hilo awe bodaboda nakuhakikishia atazunguka Sana ataona kila analofanya haliendi.

Ziko namna nyingi za kujua Kusudi nitaziweka wazi hapo baadae Kwa uchache ila Kuna mambo kadhaa nataka nidokeze kidogo kuhusu Kusudi ili hata wewe ambaye Bado hujajua uwe n shauku ya kulijua ili usiishi tu siku ziende Bali uishi unavyopaswa kuishi.

1:Urefu wa maisha yako umefungwa kwenye Kusudi.
Sitoandika vitu Ving ila nitagusia tunafahamu Kwa wasomaj wa Bible Musa alitakiwa kufa toka akiwa mtoto kwasabab watoto wa kiume wote waliuliwa lakin yeye hakufa kilichofanya endelee kulindwa ni kwasabab kulikuwa na Kusudi la kuwepo kwako

Hivyo wakati mwingne unanusulika kwenye ajali n.k ni kwasabab una Kusudi unapaswa kulitimiza na hivyo hutakufa Hadi ulifanye.

2:Umri hauzuii kulijua Kusudi maana wapo wengine wanafikr kwasb umri ushaenda haya mambo ni ya vijana no unapolijua unaanzia hapohapo lugha ya umechelewa haitokani na Mungu.

Ndio maana wapo watu unaona wazee lakin Bado wanataman kufanya mambo makubwa. Mfano Marehemu Lowasa aligombea urais hata kama umri ulikuwa unakimbia na Mali anazo ni Kusudi huwa linasukuma mtu kufanya kitu.


3:Kwenye Kusudi lako Ndio uwanja wako wa nyumbani.
Yaani hapo hata iweje kuwe na vipingamizi Gani utasimama na utaendelea mbele hutokatishwa tamaa kirahis.
4:Mungu ameiamuru baraka yako iende lilipo Kusudi lako.
Ukisoma kitabu Cha Mwanzo 12:1- utaona Abraham anaambiwa atoke kule alipoenda ndio alipoanza kuliishi Kusudi na baraka nyngi Sana alizipata akiwa katika Lile Kusudi.

5:Kusudi linauwezo wa kubadili au kung'arisha Jina.
Leo hii ukiulizwa mpiganaji maarufu wa katika list utakayotajiwa hutokosa Jina la mike Tyson. Kwahyo Jina limeng'aa kwa kile alichokuwa anafanya ambacho ndio Kusudi.

Yapo mengi siwez eleza yote ngoja nikudokeze kwenye kile ulichouliza nawezaje kujua Kusudi au purpose

Kujua Kusudi/purpose Sio jambo la siku 1 ni jambo la muda mrefu ambalo linakutaka kwanza urudi kwa aliyekufanya wewe uwepo hapa duniani Moja Kwa Moja ninaposema kurudi simaanishi ufe no namaanisha uwe na ushirika naye ili akujuze baadhi ya taarfa kukuhusu wewe.

Mfano mdogo tu unaponunua Tv au Radio huwa Kuna kijitabu kidgo ndani kunaitwa User guide au manual hiki kinakusaidia kuijua Tv au Radio hiyo na matumiz yake. Na aliyeweka hiko kijitabu ni yeye aliyeitengeneza.

Kwa mantiki hyo mm ,wewe na mwanadamu yyt Kuna aliyetutengeneza yaani kuumbwa, hivyo yeye ndio ana manual au user guide kutuhusu sisi ni lazima turudi kwake atuelekeze.

Gari iliyotengenezwa kutumia petrol ikitumia diesel nafikri unaelewa Nini kitatokea.

Sasa ngoja nikupe dondoo chache za kumsaidia mtu kujua Kusudi
Note: kujua Kusudi ni kitu kingine na kuliishi ni kitu kingine. Kwahyo Kuna waliolijua na hawaliishi na kunawasio jua wanaliishi bila kulijua

Namba Moja nilishaielekeza hapo juu kurudi kwa Mungu

2: Angalia vitu vinavyo kusumbua ukiviona na unavutwa kuvitatua.

Yaani namaanisha unaweza ukakaa mtaani kwenu ukaona Kuna jambo unaona kabisa haliko sawa lakin wenzako wengine wote wanaona la kawaida bac jua Kuna kitu unacho juu ya hilo unapaswa kukifanya.

3:Fuatilia kipi kinachovuta hisia zako kwa haraka

4:Fuatilia mawazo au ideas zinazokujia mara kwa mara.

5: Fuatilia ndoto ambazo umekuwa ukiota, si kila ndoto inatokana na uchovu ndoto ni somo Pana Sana

6:Fuatilia watu sahihi unaovutwa Sana kuambatana nao au unavutiwa na maisha yao.

Hii ya watu iko hv mara nyng ukiona Kuna mtu anakuvutia Sana ujue alichonacho hata ww unacho either hujajua au hujakifanyia kazi ili uwe kama yeye.

7:Angalia vitu unavyoweza kufanya kwa uvumilivu .yaan uko tayar kutumia hata masaa unafanya tu yaan huoni kuchoshwa.

8:Fuatilia vitu Gani unavianya kwa wepes na bila kutumia nguvu nyngi.

Mfano mdogo si umeona mm nmeandika maandishi mengi Haya Tena bila malipo yoyote na moyoni Nina furaha Sana kuandika hiki nilichoandika lakini Kuna mtu hawezi kufanya hvi


9: Angalia kiwango Cha amani na furaha unachokipata wakati unafanya kile unachokifanya.

Yapo mengi siwez andika yote lakini pia hata ukishalijua Bado Kuna mambo ya kufanya ili kulitimiza.


Nafikri Kwa sehemu naweza nikawa nimejibu kdgo
 
Wanasema kile kinachokukera na unapenda ukibadilishe. Hapo ndipo kuna kusudi lako.
 
Inahitaji nguvu kubwa au bahati
 
Binafsi sijui ila kuna story nimewahi kusikia kwamba ili mwanaume aweze kujua purpose yake lazima abstain sexual activities kwa muda fulani.

Kufanya hivyo kutamsaidia huyo mwanaume kuzi~harness hizo sexual energy na kuzielekeza kwenye his self discovery....wenyewe wanasema semen retention.

Hii itapelekea huyo mwanaume kujijua yeye mwenyewe kwanza na kujua kusudi la yeye kuwepo duniani
Hii kwa upande wangu nakataa kwasababu sex ni miongoni mwa mahitaji muhimu sana ya mwanadamu mwenye afya yake, asipopata hii huduma anakuwa hana utulivu kabisa,,, swali linakuja je utajuaje dhumuni la maisha yako kama huna utulivu ndani ya nafsi yako

Kujizuia huko lazima kutakuathiri kwa namna moja au nyingine
 
Mbona simple
Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa nyingine hizo ni blah blah tu furaha ya kweli ni kujua uhitaji wako wa kiroho hizo nyingine ni maneno za kutungwa kwa hekima za kibinadam
Sipingani na wewe unachosema ni sahihi lakini naona hii iko general sana. Kimsingi purpose ya chochote lazima liendane na misingi ya chanzo chake(chanzo cha mtu ni Mungu).

Kwa ujumla sote tuna kusudi moja la awali yaani kuwa majibu kwa ulimwengu.

Ishu inakuja kwenye kulitambua kusudi la mmoja mmoja ndo wengi bado ni giza nene, mie mwenyewe sina uhakika sana kama nipo kwenye kusudi langu hasa.
 
Mkuu,,, kama umefuatilia nimesema nimekua nikisoma vitabu na kutafuta hizo info muda mrefu kwaiyo siku nikigundua nitajua
Hivi mtoa mada hivi unatambua kama Kuna Kuna aina nne za kusudi:
1.Kusudi la MUNGU
2.Kusudi la shetani
3.Kusudi la moyo wako
4.Kusudi la watu juu ya maisha Yako

Na kupitia aina zote hizi nne ,Kila mtu huwa anajikuta anaishi kwenye aina mojawapo kutoka na sababu mbalimbali za kiroho na kimwili.
Mfano hapo kwenye namba moja ndipo huwa tunakusudiwa kuendana napo namaanisha kusudi la MUNGU,japokuwa inahitajika ufahamu wa kutosha,kujitoa na kutokukata tamaa hayo ni Kwa uchache katika kutimiza hilo kusudi

Ukija hapo kwenye namba mbili,siku zote inajulikana kwamba mipango ikipangika upande wa nuruni basi na mingine hupangwa Kwa wakati huo huo ,upande wa giza,na hapa wengi huwa tunaingia mtegoni wa kutoka kwenye njia sahihi(Kusudi la MUNGU) pasipo kujua kutokana na maisha yetu binadamu uwe tajiri au maskini,kijana au mzee huwa hayakosi changamoto na pia huwa tunategeshewa mitego/majaribu kupitia hizo hizo changamoto,Sasa wengi huwa tunakosa uvumilivu na kukata tamaa na kujikuta tunatekeleza kusudi hilo namba mbili.

Kwa hiyo namba tatu hili ndo kusudi linaloanzaga Kwa katika safari ya Kila mwanadamu na ndo huwa linaamua mwanadamu ataendana na kusudi lipi hapo baadaye kati ya Yale makusudi mawili makubwa yaani kusudi la MUNGU na kusudi la shetani,inajulikana kwamba vitu vingi kabla havijatokea au kuvifanya huwa vinaanzia moyoni,mwili ni kufanya tu kutekeleza hili na lile,Kwa mfano bunduki yenyewe kama yenyewe haiui lakini ikishikwa na mtu mwenye mwili mwenye dhamira ya mauaji moyoni huwa inatekeleza kifo mara moja
Pia chukulia na ishu zile za watu kusaidia na watu wasiowajua na huwa wanajikuta wanasema yule mtu ana moyo mzuri.

Kwa namba nne ,huwa kazi yake kuipa nguvu namba mbili,Kwa sababu shetani siku zote hutumia watu kuharibu watu Ili kusudi namba moja lisitekelezwe na mlengwa.
 
Back
Top Bottom