Guasa Ambonii
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 8,545
- 10,283
Chuma kilisepa sio na kijiji bali mataif a sijui ilikuwa foleni ya ATM au kupiga kura haki sawa kwa wote uwe tajiri au kapuku kikombe kimoja duh alikamata wengi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo huyo unae mjua ! Come on man ! Dont look at trivial errors! Debate big issues ! BAK you are better than that ! Wouldn't expect such a reaction from you !!!
Kwanini huyu mzee hakuchukuliwa hatua yeyote ile?
Kwanini aliachiwa kunywesha watu hiyo supu ya mizizi ambayo haikua imepitia vipimo na kupewa go on na mamlaka husika?
Babu Ameacha Legacy
Ambilikile Mwasapile maarufu kama Babu wa Loliondo amefariki dunia akipatiwa matibabu Kituo cha Afya cha Digodigo baada ya kuzidiwa gafla leo Mchana. Mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Ngorongoro, Waso.
Babu wa Loliondo aliugua muda mrefu na kujitibu kwa miti shamba, alipoenda hospitali akiwa amechelewa.
Babu wa Loliondo alipata umaarufu kwa dawa yake aliyodai inatibu magonjwa yote.
=======
UPDATE: July 30, 2021
Chanzo cha kifo cha Mchungaji Ambilikile Mwasapile (86) kimetajwa aliugua nimonia kali ambayo ilimsababisha kupata tatizo la upumuaji na homa.
Tangu afariki wasaidizi wake na majirani wamekuwa wakieleza kushtushwa na kifo hicho ambacho kimetokea akiwa anaendelea kutoa huduma ya tiba ya kikombe aliyoanza tangu mwaka 2011.
Mchungaji Ambilikile ambaye ataendelea kukumbukwa kwa kuvutia maelfu ya watu ndani na nje ya nchi kati ya mwaka 2011 hadi 2013 kutokana na tiba yake ya kikombe alifariki jana saa 9:45 jioni.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mangwala amesema kuwa taarifa za awali za madaktari zinaeleza chanzo cha kifo ni nimonia ambapo kwa takriban siku tano alikuwa anaumwa na kupata sindano za masaa.
"Jana asubuhi aliamka vizuri akiendelea na matibabu lakini majira ya saa nane alianza kujisikia vibaya ndipo ilitafutwa gari kutaka kumpeleka hospitali ya Wasso ambaye alitaka,"amesema
Hata hivyo amesema wakiwa wanampandisha gari alijisikia vibaya na kuanza kutapika ndipo walimkimbiza kituo cha afya Chadigodigo na alifika akiwa tayari amefariki.
Baadhi ya wasaidizi wa mchungaji Mwasapile walisema kabla ya kuzidiwa na ugonjwa alikuwa akiendelea kutoa tiba ya kikombe kwa wagonjwa kadhaa ikiwepo wa corona.
Hivi karibuni akizugumza na vyombo vya habari Mwasapile aliomba kupelekewa wagonjwa wa corona kupata tiba kwani hakuna ugonjwa ambao Mungu unamshinda.
"Wiki mbili zilizopita alikuwa vizuri anatoa tiba japo kwa watu mmoja mmoja waliokuwa wanakuja lakini hali yake iliendelea kubadilika," amesema.
James Richard jirani wa Mchungaji huyo amesema hadi anafariki hakuwa na hali mbaya na ameacha mali kadhaa ikiwepo magari, nyumba na kiwanja ambacho alikuwa anaandaa kwa kutolea tiba
"Babu bado alikuwa anasema watu watakuja Samunge maelfu kupata tiba na alipata eneo kubwa ambalo alikuwa anaendelea kuliandaa,"amesema.
Mmoja wa waliowahi kuwa wasaidizi wababu wake Poul Dudui amesema taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa kwa uratibu wa Serikali na wanasubiriwa ndugu na watoto wake kujua atazikwa wapi na lini.
James Leyani mkazi wa Loliondo, amesema msiba umetokea wakati kuna janga la corona na kuna chanjo imeanza kutolewa hivyo muhimu watu kusikiliza maelezo ya wataalam wa afya na Serikali.
"Tunakubaliana na tiba za asili na imani lakini sasa muhimu kufuata maelezo zaidi ya wataalam wa afya na Serikali ili kukabiliana na janga hili,"amesema.
Corona inaambukizwa na vimaji maji, assume umejikojolea na una chupi, je ile mikojo ina possibility gani ya kumfikia mtu aliekaa jirani yako,
Ukikohoa au kupiga chafya, vitasa vya milango na mabomba ya kushikia kwenye public transport yanaeneza haraka sana.Corona inaambukizwa na vimaji maji, assume umejikojolea na una chupi, je ile mikojo ina possibility gani ya kumfikia mtu aliekaa jirani yako,
Assume pia ungekua uchi, kuna possibility gani ya mikojo kumfikia?
Ni kweli tunaamini katika tiba mbadala lakini babu hakupewa elimu au kuandaliwa kutibu gonjwa hatari linaloambukiza haraka kama Covid.Mkuu BAK heshima kwako.
Ndiyo maana ni jambo la kheri na busara sana kuwa Chadema akiwamo mheshimiwa Mbowe kuwa wanatambua umuhimu wa chanjo hii kama kipaumbele kweli kweli.
Kumpigania Mbowe, kuipigania katiba mpya ni muhimu sana. Lakini si kipaumbele kuliko kuudunisha umuhimu wa kuzipigania hatua stahiki dhidi ya Corona tulizozifanya usiku na mchana tangia March 2020.
Mapambano yetu kuhusu lolote ni muhimu tu kama tungali hai. Responsibly "we shall define" kufikia wapi wanaotaka kuchanjwa watakuwa wamechanjwa.
Kutokea hapo kama busara itakuwa bado haichukui mkondo wake tusilaumiwe sisi. Kama ilivyo siku zote tutafanya sehemu yetu katika kuyalinda maisha ya watu wasio na hatia.
Babu Ambilikile Mwaisapile amekufa kwa kutolewa kafara na serikali ya CCM kwa maslahi binafsi ya kisiasa. Loliondo kumetolewa kafara na serikali ya CCM kwa maslahi binafsi.
1. Ni vipi babu kwa ujinga wake aliachwa kukusanya wagonjwa wa Corona Loliondo bila tahadhari yoyote?
2. Ni vipi babu wa Loliondo aliachwa kushughulika na wagonjwa Corona Bila ya kuwa na tahadhari zozote PPEs, barakoa, social distancing, maji tiririka, sabuni, wala sanitizers au chanjo?
3. Serikali na wizara ya afya waliokuwa wapi kuhakikisha mzee Ambilikile haiwezi hatarini, haweki wengine hatarini wala haiweki Loliondo hatarini?
4. Serikali inafanya nini kuona kifo na mazishi ya mzee huyu yanakuwa funzo Loliondo na kwa nchi nzima?
5. Serikali inadhani kwa kuficha sababu za kifo hiko ni kwa maslahi ya taifa hili?
Incredible!
Kwa hakika kwa vifo hivi tutawajibishana tu.
Katika list ya wahanga wale jina moja moja litakaposomwa mbele ya mumiani wale, jina la machungani Ambilikile Mwaisapile litasomwa pia.
Apumzike kwa amani Mchungaji Ambilikile Mwaisapile.
Bwana ametwaa kwa sababu ya ubinafsi waliojimilikisha utawala wa nchi hii.
Cc: Sky Eclat
Ni kweli tunaamini katika tiba mbadala lakini babu hakupewa elimu au kuandaliwa kutibu gonjwa hatari linaloambukiza haraka kama Covid.
Inatia kichefu chetu. Kwamba "bwana alitoa, bwana ametwaa jina lake LIHIMIDIWE?! Aaah wapi!