Ambrose Dunga: Producer aliyezivunja vunja Bongo Records, MJ Records kwa ma-beat makali yenye 'back vocals'

Nako 2 Nako, Weusi pia kawapatia sana

MANDUGU DIGITAL NI BALAA

DUNGA ANAJUA AISEE TUMPE CREDITS ZAKE.... KWENYE TOP TEN YANGU YA MUSIC PRODUCERS YUPO
 
Kwenye wimbo wa MANUVA wa Joh Makini..

Mwishoni Joh anasema -: DUNGA UTAWAUA..
Dunga anajibu -: MY CONDOLOSENCE..

Jamaa alikuwa na swagger sana..

Msafwa,
Uporoto, Mbeya..
 
Hii ndio raha ya JF


Mkuwe unaweka nyuzi ka hizi kila siku.

 
Dunga pia alifanya kazi ya Nikki Mbishi feat Collo na V-Money inaitwa Toast to life Collo na V-Money, ambapo track hiyo imetumiwa kama reference na P the MC kwenye futi 6 kumshangaa Nikki kwa nini hakutusua licha ya kupata collabo na wasanii wakubwa tena waliopo katika chart kwa nyakati hizo. Ilikuwa ni Collabo isiyotegemewa kufanywa na msanii kama Nikki Mbishi.

Pia alifanya ile ngoma tamu ya Enika inaitwa Changanya Changanya - background vocals zake " Mama eeh ohaa"

Joh Makini alifanyiwa mikono hatari kama Chochote Popote, Zamu Yangu na Manuva

TMK wanaume ile kazi ipo ukichanganya na ile kutengana kwao iliwatingisha kwelikweli kina Juma Nature (TMK Asilia), ile beat iliwafanya wakune sana vichwa namna ya kurudisha mashambulizi.

Kwa kweli umefanya uchambuzi vyema sana, umerudisha kumbukumbu wakati muziki ukiwa muziki.
 
Iyo Baba Style Ya Noorah Asee Si Mchezo Beat Yakee---
Jamaa Aligonga Base Apo[emoji3][emoji3]


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hii ngoma nimeitafutaga sana sijaipata aisee, mwenye nayo ninaomba anitumie hapa au kwa PM au hata kama ni link. Ngoma kali sana ile aisee
 
Hivi producer effector na ile lebo yake nimeisahau jina yuko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Studio ilikuwa inaitwa Serious Records ilikuwa Maili moja Kibaha nadhani. Alikuwa ndio Chief Producer akisaidiana na Marco Chali pamoja na Amba. Effector alifanya kazi kali hizo za ECT, alifanya kazi na Pig Black, akafanya ngoma ya Dark Master feat Ngwair inaitwa Dark master pia. Baadae studio ilikufa maprodusa wakatawanyika, Marco Chali nafikiri ndio akaenda Kama Kawa records ya G Solo na Amba kafungua studio yake AB records Iringa, Effector kama sikosei alikwenda tena kusoma mambo ya Sound South Africa.
 
Katika production za miaka ya karibuni nimeielewa sana ngoma yake Say Something aliyo feature na Drake.
Pia kuna moja aliitoa 2016 hivi inaitwa Dont Get No Betta, ni kali sana ina beat moja tamu sana
 
Jina la yule jamaa alikuwa anaitwa Stan Boy, kuna video aliiweka youtube mwaka 2009 akiwa USA, alikuwa anatangaza muziki wake na kusema unapatikana myspace.com ambayo kwa sasa haipo file zilikuwa corrupted zote na tovuti ikafa kabisa (hata mimi nilipoteza baadhi ya kazi zangu huko). Ukiangalia video anasema pia anapatikana facebook na site nyingine

Mbali ya track za ECT kama crew pia alifanyaga collabo na AY ile track ya mademu watafutaji
 
Ndio maana wanakushutumu kuwa wewe ni dume tena la mbegu, mwanamke anachambuaje muziki namna hii!

Au Modds mnasemaje?
Kama kweli ni mgonga code. Weledi wake wa uchambuzi unashabihiana kabisa. Hivyo anaweza kuwa ni mwanamke. Kiufupi ukishakuwa mtu wa code anakuwa na uelewa mpana wa jambo ambalo anakuwa na interest nalo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timbaland ana mabalaa, anaujua muziki mpaka amepitiliza. Nafikiri ndio producer aliyeanza kutoa sample za kutumia mdomo wake (human sound) na zikawa kama accoustic safi kabisa kwenye wimbo. Mbali ya hiyo alikwa anafanya Dj-ing skills ya kuchezea nyimbo au kupandishia na wakati huo music software hazikuwa na effects au automation za kufanya kwa urahisi mambo hayo. Kuna track ya Get your Freaky On ya Missy Eliot, beat inapokaribia kumalizika anapandishia kama mara 3 hivi beat ya BUBBA SPARXXX - Ugly ambayo nayo kaitengeneza yeye mwenyewe, dah fleva yake sio ya kitoto. Wakati ule muziki wa Hip Hop umepata Crunk kama sub genre alikuja kutengeneza track ya 50 Cents ft. Justin Timberlake - Ayo Technology, zile appregiations anazijua mwenyewe na bado mwishoni ckaichezea chezea beat na kuirudisha kwenye melody ya awali, Hapo kuna ilre track ya The Game inaitwa Put you on the game, nayo alifanya beat hatari na akaichezea chezea ki-Dj. Halafu ametoka kutoa midude mikavu ya HipHop ghafla anaswitck kukupa Rehab ya Rihanna, kuna gitaa tamu sana kama lile la What's Goes Around Comes Around ya Justin Timberlake...

Tuliowahi kutumia Fruity Loops 3 moja ya tutorials ilikuwa ni beat ya Try Again ya Aaliyah..Na ukitaka kujipa stress na kukata tamaa ilikuwa uisikilize hiyo beat halafu ufananishe na unazotengeneza, unaona kama Image-Line wanataka kuua hivi, unabaki kujiuliza huyu Timbaland alifanyaje beat kama hii, mbona haiwezekani kabisa kufanywa.

Itoshe kusema Timbaland ni zaidi ya Music Producer, sio mtu wa kawaida.
 
Respect sajo

Unaweza kuwa na Sweet girl ya huyu Stan Boy?

Pia pole kwa kupoteza kazi zako sheikh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ebwana eeeh track ya ya 50 ile ya ayo technolog ninyokooo balaa tupuuu....
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwa maelezo haya, sajo unaujua muziki.
Respect kaka. Usiwe kama @RHONDO, yeye amekazania kujua magari na pafyumu tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…