Timbaland ana mabalaa, anaujua muziki mpaka amepitiliza. Nafikiri ndio producer aliyeanza kutoa sample za kutumia mdomo wake (human sound) na zikawa kama accoustic safi kabisa kwenye wimbo. Mbali ya hiyo alikwa anafanya Dj-ing skills ya kuchezea nyimbo au kupandishia na wakati huo music software hazikuwa na effects au automation za kufanya kwa urahisi mambo hayo. Kuna track ya Get your Freaky On ya Missy Eliot, beat inapokaribia kumalizika anapandishia kama mara 3 hivi beat ya BUBBA SPARXXX - Ugly ambayo nayo kaitengeneza yeye mwenyewe, dah fleva yake sio ya kitoto. Wakati ule muziki wa Hip Hop umepata Crunk kama sub genre alikuja kutengeneza track ya 50 Cents ft. Justin Timberlake - Ayo Technology, zile appregiations anazijua mwenyewe na bado mwishoni ckaichezea chezea beat na kuirudisha kwenye melody ya awali, Hapo kuna ilre track ya The Game inaitwa Put you on the game, nayo alifanya beat hatari na akaichezea chezea ki-Dj. Halafu ametoka kutoa midude mikavu ya HipHop ghafla anaswitck kukupa Rehab ya Rihanna, kuna gitaa tamu sana kama lile la What's Goes Around Comes Around ya Justin Timberlake...
Tuliowahi kutumia Fruity Loops 3 moja ya tutorials ilikuwa ni beat ya Try Again ya Aaliyah..Na ukitaka kujipa stress na kukata tamaa ilikuwa uisikilize hiyo beat halafu ufananishe na unazotengeneza, unaona kama Image-Line wanataka kuua hivi, unabaki kujiuliza huyu Timbaland alifanyaje beat kama hii, mbona haiwezekani kabisa kufanywa.
Itoshe kusema Timbaland ni zaidi ya Music Producer, sio mtu wa kawaida.