Ambrose Dunga: Producer aliyezivunja vunja Bongo Records, MJ Records kwa ma-beat makali yenye 'back vocals'

Ambrose Dunga: Producer aliyezivunja vunja Bongo Records, MJ Records kwa ma-beat makali yenye 'back vocals'

"The Rain (Supa Dupa Fly)" by Missy Elliott sampled Ann Peebles's "I Can't Stand the Rain". Hii ndio Moja kati ya ngoma Kali nazozielewa kutoka kwa Missy Elliot.
Hii ngoma pamoja na ile ya Aaliyah "Are you that somebody" hua ni shidaa. Infact karibu nyimbo zote kali za Aaliya na Miss Eliot aliproduce Timba.
 
Huyu jamaa ilikuwa hatari nyingine japo ujuzi wake ulikuwa haulandani na muonekano wake! 😂😂😂

Alisababisha ugomvi wa Q Chilla na Jafarai enzi hizo! Chilla aliurudia wimbo (remix) wa My Boo (kama sijakosea jina) ambao original yake ilikuwa ya Jafarai akimshirikisha Chilla.

Dunga kitu alichokuja kukifumua ni hatari tupu plus na Chilla nae alikuwa kwenye peak ya ujuzi wake!

Waliifunika original version ya Jafarai masikini! Nilisikia sikia kuwa Chilla aliamua kufanya hivyo sababu walipishana terms na Jafarai baada ya kumaliza kumfanyia kazi (hakumlipa 😂😂😂)!
Hapo kwenye muonekano ni kwamba tumezoea kuwaona wanaohusika kwenye tasnia ya burudani wanakuwa wamepiga pamba flani hivi na swagga kibao

Yaani hata mie nilikuwa nasikia ukubwa wa Dunga those days na wakati mwingine hata kumwona Dunga kwenye video ila nilikuwa sidhani kama yule wa kwenye video ndio Dunga

Kwenye wimbo wa Matonya wa ANITA unaweza ukasema msela flani tu wa kitaa hasa wimbo unapomalizikia wamekaa kwenye gogo I think
 
Na kuna Bwana anaoitwa Lindu, alikuwa mtayarishaji wa muziki wa hiphop miaka ya 2000s, sijui kama mpaka sasa bado anendelea na kazi hiyo. Alikuwa ni mwenye mwili sana (mnene) na anaonekana kama mzembe mzembe ila beat zake sasa ni balaa, moja ya kazi yake ni hii alifanya na Chid benz inaitwa natubu (2005)
 
Jana usiku wakati nachapa code za JavaScript (hii language siipendi basi tu!!) huku nasikiliza album ya Joyner Lucas -ADHD kuna wimbo mmoja unaitwa 10 Bands uli-popup. Ndani ya ngoma hii ameshirikishwa the Legend Producer Timberland.

View attachment 1451643

Kwa ambao hamumjui producer Timberland tafuteni ngoma za marehemu Aaliyah (sio huyu wa Wasafi), Aaliyah msanii aliyefariki kwa ajali ya ndege akiwa na crew yake wakitoka ku-shoot video ya "Rock the Boat" kule visiwa vya Bahamas. Karibu 98% ya nyimbo za Aaliyah zilitengenezwa na legendary Timbeland 'Mzee wa Back vocals'.

Karibu nyimbo zote alizotengeneza Timberland, kuna kitu 'common' na very 'unique' kwenye beats za Timberland, zile 'back vocals' ambazo alikua anaimba Timberland mwenyewe. Okey tufanye hivi, tafuta nyimbo zifuatazo sikiliza halafu utagundua nachoongelea:

Aaliyah - Try Again
Aaliyah - Are you that somebody
Aaliyah - More than a woman
Justin Timberlake - My love
Missy Elliott - Get Ur Freak On (Napenda zile back vocals 'Piki piki donsee')
Ginuwine - Same OL G (Aisee ukiwa na stress sikiliza hii ngoma, Timberland nyoko!!)

Sikiliza beats za hizo nyimbo hapo juu. Umesikia hizo back-vocals? Basi huyo ndio Timberland mzee wa ma-beat!

Hii ikanikumbusha miaka ya 2004 mpaka 2012 kipindi Bongo Records na MJ Records bado wanatawala 'music production industry' ya Bongo, kuna producer Mkenya alikuja kuleta mapinduzi akawavunja vunja kina P-Funk Majani na Master Jay wakapotea kwenye production ya muziki wa Bongo-Fleva mpaka kesho!!

Unakumbuka miaka ya 2005 - 2010 karibu kila ngoma mpya ya Bongo-Fleva unasikia wanataja "Mandugu Digitoooo" au wakati mwingine unasikia "41 Recordssssss". Kama umesahau basi sikiliza ngoma ya Prof. Jay "Hapo Vipi" au ngoma ya Mwasiti na Chid Benz "Hao" utasikia hizo jingles. Nyuma ya pazia alikuepo 'Timberland wa Bongo' Ambrose Dunga.

Jamaa kwa muonekano ni kama mshamba mshamba hivi, lakini kazi zake zilikuwa ni nyoko!

Unaikumbuka ngoma ya Nakaaya - Mr. Politician? Basi yule 'Mr. Politician' kwenye video ndio Producer Dunga huyo! Unacheki alivo na msuti ule!! Mshamba kweli.

View attachment 1451649

Fanya hivi, angalia video ya Matonya - Anita pale beat linaanza yule anasema "Tusichongole chongole" ndio Producer Dunga huyo. Umecheki anavookena mshamba na hilo Tishet lake la njano nyuma ya nyumba yenye ukuta wa tofali za kuchoma halafu inataka kubomoka?

View attachment 1451647

Ikafika kipindi wasanii wote waliokua wateja wazuri wa Bongo Records na studio zingine wakawa wanamiminika Mandugu Digital. Producer Lamar nae akaona isiwe tabu, akamkimbia P-Funk ajifie na Bongo Records yake akaenda kuongeza maufundi kwa Producer Dunga. Aisee Lamar na Dunga waliunda 'Duo" moja kali sana.

Akina Prof. Jay wakaona isiwe tabu, wakafuata midundo yenye "back vocals' kwa 'Timberland wa Bongo'. Marehemu Ngwair aliyekua msanii 'Loyal' kwa P-funk na yeye akaona isiwe tabu. Kwanza alikua ameshapotea hasikiki tena, lakin alivoenda kwa 'Timberland wa Bongo' ndipo akaja na "Nipeni Dili Masela" ndio akarudi kwenye mainstream. Hii ngoma ukisikiliza zile 'back vocals' za Dunga utaelewa kwanini Dunga namfananisha na "Timberland wa Aaliyah"

Chini ni baadhi ya ngoma zilizopikwa na producer Dunga akisaidiwa na Lamar (kabla ya kuiva na kuunda 'Fish Crab'):

1. MB Dogg - Natamani (Kule mwishon Dunga anaimba "dumba dumba dumba dumbe")
2. Mwasiti ft. Chid Benz- Hao (Utamsikia Dunga anaimba "Tunadunda dunda duundaaa")
3. Nakaaya - Mr. Politician (Utamsikia Dunga "Nipeni kura zenu.. Nivotieni.. Put your hands up")
4. Prof Jay - Hapo Vipi
5. Ngwair - Nipeni Dili
6. Nako 2 Nako ft Loon - Bayeyo (beat linadunda hili ni nyoko)
7. Matonya - Anita (Tusichongole chongole)
8. Noorah - Baba styles
8. Ngwair ft. TID - She Performs ("Thi..This should be played at high volume")
9. Temba ft. Ray C - Nipe Mimi
10. Fatma ft. Jay Moe - Chozi la kusimuliwa

Kila kitu kina muda wake. Nani anaikumbuka match ya EPL iliopewa nickname ya "Battle of the Buffet"?

October 29, mwaka 2004 katika uwanja wa Old Traford, mabao mawili kutoka kwa Ruud van Nistelrooy na Wayne Roon yali-hitimisha "49 unbeaten record" ya washika mtutu wa London Arsenal. Mechi hiyo ilitawaliwa na vurugu kama zoteee. Hadi kupelekea Cesc Fabregas kumrushia kipande cha Pizza kocha Alex Ferguson wakat wanatoka uwanjani. Na ndio sababu ya mechi hiyo kubatizwa "Battle of the BUffet".

Leo hii May 16, 2020 mechi kati ya Man U na Arsenal inaonekana kama Aston Villa anacheza na Norwich. Mechi haina tena impact. Hakuna ile amsha amsha kama ya 2004.

Kila kitu na muda wake. Battle of the Buffet imehamia kwa Man City vs Liverpool.

Producer Dunga hatimaye (sijui kwa sababu zipi) alisepa Bongo akarudi kwao Kenya.

Lamar nae akafungua Studio yake Fish Crab. Uzuri akaendeleza ufundi aliopata kutoka kwa 'Timberland wa Bongo' kwa kutengeneza beats za kipekee zenye identity, zenye "back vocals' na jingles. Ukisikia tu "Talk of the town... Lamar.. Aaaaaaaaauu" unajua huyu ni Lamar.

Siku hizi mambo yamebadilika. Hakuna tena 'monopoly' ya music production.

Studio na Producers wamejaa Bongo yoteee... Hakuna tena 'Timberland wa Bongo' kama ilivokua miaka hiyo.

Ngoja niendelee kusikiliza ngoma za Joyner Lucas hapa, kuna ngoma inaitwa Will. Anamsifia na kumu-appreciate mwanamuziki na muigizaji Will Smith akielezea kuwa Will Smith ndio 'Role Model' wake tangu enzi hizo Joyner Lucas ana struggle kutoka.

Ingia Youtube search Joyner Lucas - Will, uone alivojivika uhusika kwenye movies za Will Smith alizoigiza zamani!!

-------- UPDATES--------
Kuna mdau kachangia amesema Dunga yupo Tanga bado anafanya production (japo sio intensive kama enzi zile). Nimeangalia video ya msanii Galatone - Samaki (ipo Youtube) nimemuona Dunga kama kawaida yake na 'back vocals' 😀 😀😀😀
View attachment 1451874


-------------UPDATES 2--------------
Asante mdau josephmasamaki kwa kunipa update nilikua sijui kama ngoma ya Chege na Temba - Go Down ya mwaka 2017 imetengenezwa na Dunga. Nimeicheki Youtube 'back vocals' zake kama kawaida. "Mama yanguuu.. Tembelee"
Dunga ananifurahisha sana halafu amekula suti kaliii 😀 😀😀
View attachment 1452188

Mama Debora
Nimekoshwa na uandishi na upangiliaji wa facts, jamaa hakuwah waacha maproducer salama wakaishia kumfanyia visa,figisu na mwishowe hadi kumroga akaona isiwe kesi akaachana na tasnia kwa muda akarud kwao Kenya baada ya muda ndo karud tena bongo kuendeleza harakati zake cjui alienda kujipanga kivingine?
 
Na kuna Bwana anaoitwa Lindu, alikuwa mtayarishaji wa muziki wa hiphop miaka ya 2000s, sijui kama mpaka sasa bado anendelea na kazi hiyo. Alikuwa ni mwenye mwili sana (mnene) na anaonekana kama mzembe mzembe ila beat zake sasa ni balaa, moja ya kazi yake ni hii alifanya na Chid benz inaitwa natubu (2005)


Unamkumbuka producer mmoja alikua anaitwa Prof. Ludigo.
Alitengeneza sana kazi za kina John Walker Wagosi wa Kaya.
Alipoteleaga wapi.
 
Walishuti Morogoro. Kitongoji kinaitwa Bigwa. Yule mzee anae onekana na Baskeli alikua anuzaga mkaa, na walimlipa 10000 kwa kazi ile aliyoifanya...!

Sent using Jamii Forums mobile app

Unafikiri Kwanini Matonya haku-make na kudumu kwenye game kama Diamond Platnumz! Maana alikuaga yuko on fire sana.
 
Najiuliza hapa vipi YouTube haiwezi files ku-corrupt na kila kitu kupotea?

inawezekena, lakin probability ni 0.002%.
Google wame-invest a lot of money YouTube. Kifupi YouTube ndio money making machine ya Google.
It's obvious wanazingatia all precautions kuepukana disaster kama hiyo itokee
 
inawezekena, lakin probability ni 0.002%.
Google wame-invest a lot of money YouTube. Kifupi YouTube ndio money making machine ya Google.
It's obvious wanazingatia all precautions kuepukana disaster kama hiyo itokee
Bila shaka wana back-ups za kufa mtu.
 
Ila P funk majani (bongo records), Royi(G-records), pia mika mwamba ilikuwa shida zaidi ya huyo dunga, kwa sasa wapo vijana wazuri tu wanagonga vinanda mfano...S2kizzy, Lizer, Blacky ni shidaa
 
Iyo Baba Style Ya Noorah Asee Si Mchezo Beat Yakee---
Jamaa Aligonga Base Apo[emoji3][emoji3]


Sent from my iPhone using JamiiForums
Daaah nilikuwaga najiuliza hilo dude kaligonga nani kumbe ni dunga aisee ile ngoma kwa mfano naanza hivi, nazunguka zunguka usidhani ni rahisi......................
 
Ila P funk majani (bongo records), Royi(G-records), pia mika mwamba ilikuwa shida zaidi ya huyo dunga, kwa sasa wapo vijana wazuri tu wanagonga vinanda mfano...S2kizzy, Lizer, Blacky ni shidaa
S2kizzy ni habari nyingine aisee, hadi P funk alimtaja kwaw vijana wanaotisha kwa mabeat...
 
Daaah nilikuwaga najiuliza hilo dude kaligonga nani kumbe ni dunga aisee ile ngoma kwa mfano naanza hivi, nazunguka zunguka usidhani ni rahisi......................

Afu Mbona Silioni Youtube??
 
Dunga pia alifanya kazi ya Nikki Mbishi feat Collo na V-Money inaitwa Toast to life Collo na V-Money, ambapo track hiyo imetumiwa kama reference na P the MC kwenye futi 6 kumshangaa Nikki kwa nini hakutusua licha ya kupata collabo na wasanii wakubwa tena waliopo katika chart kwa nyakati hizo. Ilikuwa ni Collabo isiyotegemewa kufanywa na msanii kama Nikki Mbishi.


Pia alifanya ile ngoma tamu ya Enika inaitwa Changanya Changanya - background vocals zake " Mama eeh ohaa"


Joh Makini alifanyiwa mikono hatari kama Chochote Popote, Zamu Yangu na Manuva

TMK wanaume ile kazi ipo ukichanganya na ile kutengana kwao iliwatingisha kwelikweli kina Juma Nature (TMK Asilia), ile beat iliwafanya wakune sana vichwa namna ya kurudisha mashambulizi.

Kwa kweli umefanya uchambuzi vyema sana, umerudisha kumbukumbu wakati muziki ukiwa muziki.

Bila kuisahau na "Kichaa Cha Mbwa"
 
Back
Top Bottom