Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Hivi ni wangapi wanatambua kuna miito tofauti ya ving'ora vya taarifa za tahadhari na dharura?
- Kuna muito wa king'ora cha dharura ya moto
- Kuna muito wa king'ora cha mgonjwa aliye mahututi ama anayehitaji matibabu ya haraka
- Kuna muito wa king'ora cha polisi ama jeshi (kukiwa na watuhumiwa hatari ama hali ya hatari)
- Na kuna muito wa king'ora cha kiongozi
Mjadala wangu unajikita kwenye muito wa king'ora cha gari la kubebea wagonjwa mahututi ama wanaohitaji matibabu ya haraka, na wahudumu wa chumba cha mahututi, chumba cha dharura.
Kwenye hili niwapongeze sana madereva wale wa zile gari za kubebea wagonjwa mahututi. Wako vizuri, wanajitoa na wana UTHUBUTU na nia ya dhati ya kumwahisha mgonjwa panapostahili kwa ajili ya kuokoa maisha yake.
Changamoto ziko hapa
1. Gari husika. Ndani hakuna vifaa muhimu ama vya kutosha kwa matumizi ya dharura wakati wa kumhamisha mgonjwa sehemu moja hadi nyingine.
2. Barabara zetu. Nyingi ni finyu zenye misururu mirefu ya foleni huku tukiwa hatuna barabara za dharura
3. Uelewa wa wananchi na madereva wengine. Dereva anaona kabisa linalokuja nyuma yake ama mbele yake ni gari la wagonjwa na vimulimuli na ving'ora lakini haoni umuhimu wa kulipisha ama kulipa njia.
4. Wahudumu wa chumba cha mahututi, chumba cha dharura. Hapa ndio utajua kuwa kuna watu hawajali kabisa maisha ya wengine. Hapa nawaongelea wahudumu wale wa kwanza kumpokea mgonjwa toka kwenye gari na kumuingiza kwenye chumba cha mahututi ama dharura. Hawa hawathamini kazi kubwa na ya hatari iliyofanywa na dereva hadi kufika hapo salama. Sizilengi hospitali za binafsi.
Uzembe mkubwa na kutojali uko kwenye hospitali za serikali na vituo vyake vya afya. Mifano ni mingi lakini wa wazi kabisa ni pale Muhimbili, hospital kubwa ya Taifa ya kutumainiwa. Wahudumu wale ni wazito ni wazee ni wanene wasiojiweza. Kama wamebadilishwa basi ni sasa. Mapokezi nazo ni changamoto kubwa. Wagonjwa mahututi hawapewi umuhimu wanaostahili.
Hili la uelewa wa madereva wengine lilimfunza dereva mmoja somo kubwa lakini lililojaa maumivu makali. Mkewe alikuwa mjamzito wa mapacha, jamaa ni dereva wa daladala Buguruni Posta. Siku ya siku mkewe akazidiwa usiku mwingi hivyo jamaa akafanya namna na kumkimbiza Amana hospitali. Ilipofika alfajiri akamuacha mgonjwa anahudumiwa, akaenda kuamsha.
Trip ile ya kwanza kupita Amana hospitali kwa mbele tu kidogo ikaja ambulance ya Amana hospitali ikiomba njia, jamaa hakujali kabisa pamoja na kelele za abiria kuwa anachofanya sio kizuri. Hatimaye ambulance kwa shida sana ikapata upenyo na kuondoka.
Mida ya saa mbili asubuhi akiwa Posta anapakia kurudi Buguruni anapokea simu ya kifo cha mkewe pamoja na mapacha wake, lakini lawama zikielekezwa kwa dereva wa daladala aliyemchelewesha mgonjwa kwa kukataa kutoa njia.
Nina mifano mingi. Mingine inanihusu kabisa na mingine nimeishuhudia kwa macho yangu.
Sekta hii ya afya hasa kitengo cha dharura na mahututi kwenye hospitali za serikali bado hakijapewa kipaumbele na umuhimu unaotakikana. Kila kitu kwetu ni SIASA. Tulipokosea pakubwa ni pale tulipoamua kuupa ujuzi kisogo na kuipa siasa thamani kubwa.
NB: (Nota Bene) Mimi siko Jeneva niko Msata Kilingeni.
Jr[emoji769]