Nilifika hosp moja ya mkoa mkewangu wali fanya uzembe kumzalisha mpaka jioni akawaameishiwa nguvu..ikabidi ni force apewe refar katika hosp ya wazazi mimi nilikatisha njia chaajabu nilifika sawa na ambulance.chaajabu hao wamapikezi wa emergency walipomuona wanashusha bila kuuliza tatizo mama mmoja anasema mkewangu achuchumae aruke uchura..lkn nilimuomba sana Mungu anihepushie hasiraa...bado mtoto huyo akazaliwa..baada ya miaka minne akaungua mgongo tukaenda zahanati ya jirani na ninapo ishi wakanipa refer kwenda hosp ileile ya mkoa walipo fanya uzembe..wakati wakujifungua Dr akanipa risit ya mtoto mwingine inajina la yule mtoto nikanunue dawa sikujari nikasema moyoni kuwa kwakuwa kaona mtoto ameungua sana ndiomaana kanipa risit ya yule mtoto tuokoe muda maana angeanza kuandika muda ungeenda...kwasababu case nimoja kaona anipe hiyo..nikakimbia dukani japo mbali nikitetea uhai wamtoto
ilikuwa saa 2 usiku..naalisema ahudumiwi mpaka nirudi nikafanya hivyo nilipo rudi namkuta mkewangu anatoka machozii tuu nika wapa manurse dawa..wakaenda muita Dr alichojibu akasema anaangalia taarifa ya habari ya michezo mpaka iiishee nurse kwa huruma akasema kama alivyo ambiwa ilituuma sanaa..nilijikaza aalipo maliza tena yeye hakuudumia mtoto akasema manurse wamuhudumiie hapo ndipo nikaambiwa turudi tutakuwa tunamsafisha na maji ya chumvi nyumbani baada week 2 ndio turudi...lkn baada ya siku 5 mtoto akaanza kukunja miguu nakuremaa tusijue ilipo fikia week nakitu akaanza kuoza mgongo tukaelekezwa hosp moja hivi ya mzungu inaitwa kwa lena ipo ifisi..pale sikusema kuwa nilimpeleka mtoto hosp lengo wampokee. Maana wangekataa walinifokea sanaa nakusema kidonda nikikubwa hatunauwezo wakukiuguza nyumbani lkn nilipiga kimya kujishusha mtoto atibiwe kesho yake mtoto akapata huduma jioni mkewangu ananipigia cm mtoto amesimama nilimshangaa sana Mungu. Baada yasiku 4 tukaruhusiwa tulihudhuria kwa muda wa mwezi kusafisha kidonda na mtoto akapona niliandaa zawadi kwa wahudumu wale nikawapelekea japo walikataa lakini niliwaomba wapokee huku machozi yakinitoka ndipo wakapokea haikua pesa..baada ya mwaka yule Dr alifukuzwa kazii aliyekua anaangalia tv..alihukumiwa na sheria ya asili..
Mshana Jr umenikumbusha mbali nimeumia tenaa..