The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mwanamuziki wa Gospel kutoka Ambwene Mwasongwe ametokea hadharani na kuwaomba radhi watu wote walio chukizwa na kitendo cha yeye kutokea katika jukwaa la siasa.
Ambwene ameomba radhi na amefafanua kwa mgombea aliyekwenda kumuunga mkono ni jamaa yake wa siku nyingi na alimualika katika ufunguzi wa kampeni hizo za ubunge.
Yeye kama jamaa wa karibu wa ndugu huyo alialikwa kuimba na kwa wakati ule hakuona kama ni shida maana aliamini alikuwa akishiriki jambo la kijani kwa jamaa yake. Lakini baada ya jumbe nyingi za wadau na wapenzi wa mziki wake amegunduaaliteleza na ameomba radhi.
Pia ametoa nafasi ya kuwasikiliza watu walioumizwa na tukio hilo akitoa nafasi ya kueleza hisia zao kwa lugha nzuri yenye staha.